-
Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video za kufurahisha na kuvunja mbavu. -
Video mpya ya Staa mwingine wa Bongofleva Dogo Janja ambayo inafatia ‘ukivaaje unapendeza’ -
Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video za kufurahisha na kuvunja mbavu. -
Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video za kufurahisha na kuvunja mbavu. -
Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video za kufurahisha na kuvunja mbavu.
Showing posts with label Mtembezi. Show all posts
Showing posts with label Mtembezi. Show all posts
Friday, October 14, 2016
Tuesday, October 11, 2016
POLISI WAKAMATA MTANDAO WA SCORPION
POLISI Kanda Maalumu ya Dar es Salaam imefanya operesheni katika maeneo ya katikati na pembezoni mwa Jiji la Dar es Salaam na kuwakamata watuhumiwa 87 wa makosa mbalimbali, wakiwemo waliokuwa kwenye mtandao wa uhalifu wa mkazi wa Machimbo Yombo jijini Dar es Salaam, Salum Njwele (34) maarufu kama ‘Scorpion’.
Njwele alifikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala mwishoni mwa wiki, kujibu mashitaka ya unyang’anyi wa kutumia silaha na kumtoboa macho yote mawili Said Mrisho.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Kamanda wa Kanda hiyo, Kamishna wa Polisi Simon Sirro alisema watuhumiwa wengine wanadaiwa kuvunja nyumba na kuiba na wengine walipatikana na gongo lita 148, bangi kete 95 na puli 48.
Alisema watuhumiwa hao, wamekamatwa kwa nyakati tofauti katika maeneo ya Mbagala, Buguruni, Kiluvya, Gongo la Mboto, Tandika, Ukonga, Banana, Kunduchi, Keko, Kawe.
“Watuhumiwa hao walipatikana na makosa mbalimbali yakiwemo kuvunja nyumba usiku na kuiba maarufu 10 ndani 10 nje, kuvuta na kuuza bhangi, kuuza na kunywa gongo, kupiga debe, uzembe na uzururaji,” alisema Kamanda Sirro.
Jiunge na hatukwamii.blogspot.com/ sasa
Monday, October 10, 2016
JPM- WATANZANIA WAFICHUENI WAVURUGA AMANI
RAIS John Magufuli amewataka watanzania kuwa mstari wa mbele, kutunza amani yao kwa kuhakikisha wanawafichua wale wote wenye lengo ya kuivuruga amani hiyo.
Pia, ametoa changamoto kwa vyombo vya habari nchini kuweka zaidi uzalendo mbele na kuandika habari za maendeleo ya nchi zinazoonekana, badala ya kung’ang’ania kuandika habari zenye mlengo wa kuiponda serikali pekee.
Rais alisema hayo mwishoni mwa wiki, wakati akizindua kiwanda cha kusindika matunda kinachomilikiwa na kampuni ya Food Products ya Bakhresa kilichopo katika Kijiji cha Mwandege wilayani Mkuranga mkoani Pwani.
Alisema endapo Watanzania wataichezea amani iliyopo iliyodumu kwa muda mrefu, jitihada za serikali za kuijenga nchi kiuchumi na kimaendeleo ikiwemo uchumi wa viwanda, kamwe hazitazaa matunda.
“Navipongeza vyombo vya dola kwa jitihada zake za kuhakikisha nchi inadumu kwenye amani, nawahakikishia serikali haitovumilia mtu yeyote mwenye nia ya kuivuruga amani hii,” alisisitiza.
Alifafanua kuwa Tanzania ni moja kati ya nchi zinazozungumziwa kuwa uchumi wake kuwa unakua kwa kasi barani Afrika; huku uchumi wake katika robo ya pili ya mwaka pekee ukifikia asilimia 7.9.
“Lengo la serikali yangu ni kuhakikisha uchumi unakua na kufikia asilimia 7.2 lakini hadi robo ya pili ya mwaka tumefikia asilimia 7.9 tumevuka lengo. Hii ina maana kuwa mpaka tufikie robo tatu hata kama hapo katikati kutatokea mgogoro kidogo wa kiuchumi tutaweza kufikia lengo la asilimia 7.2,” alisema.
Jiunge na hatukwamii.blogspot.com/ sasa
Friday, October 7, 2016
WANAFUNZI WA SHULE ZA MSINGI KUANZA KUSAJILIWA KIELETRONIKI
BARAZA la Mitihani Tanzania (Necta) limeunda mfumo wa kutunza taarifa za wanafunzi wa Shule za Msingi (PReM), ambao utasaidia katika uandikishaji wa wanafunzi wote na kupewa namba maalumu, ambayo itamtambulisha mwanafunzi katika ngazi mbalimbali za mafunzo na hivyo kuondoa tatizo la wanafunzi hewa.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, jijini Dar es Salaam kuhusu mafanikio ya baraza hilo, Ofisa Habari wa Necta, John Nchimbi alisema mfumo huo pia utasaidia katika uhamisho wa mwanafunzi kutoka shule moja hadi nyingine ndani ya mkoa au nje ya mkoa.
Alisema mfumo huo utarahisisha utaratibu unaotumika sasa wa kuhamisha mwanafunzi kutoka shule moja hadi nyingine na kuweza kuondoa tatizo la wanafunzi hewa na pia utasaidia katika uandaaji na utoaji wa takwimu za wanafunzi katika ngazi ya shule, wilaya, mkoa hadi ngazi ya Kitaifa.
Aidha, alisema mfumo huo utasaidia katika ufuatiliaji wa taarifa za matokeo ya kila mwanafunzi ili kuhakikisha wadau mbalimbali wa elimu wanapata ufahamu wa kutosha kuhusu ufundishaji na ujifunzaji katika ngazi ya shule.
Alisema baraza limeanza kufanya majaribio ya mfumo huo katika mikoa miwili ya Mwanza na Ruvuma na ifikapo Desemba mfumo huo utaimarishwa ili Januari hadi Mei mwaka 2017, utumiwe na mikoa yote kusajili wanafunzi wa shule za msingi.
“Mfumo huu utadhibiti sana udanganyifu kwa sababu kila mwanafunzi anapoanza shule atapatiwa namba ambayo ataendelea nayo hiyo hiyo katika elimu ya sekondari kidato cha nne hadi cha sita…mfumo huu utakuwa na picha hivyo kudhibiti udanganyifu,” alisema.
Jiunge na hatukwamii.blogspot.com/ sasa
Thursday, October 6, 2016
“WIZKID NA DIAMOND KUKUTANISHWA NA PRODUCER HUYU”
DK SHEIN- ULINZI UIMARISHWE KATIKA KISIWA CHA UNGUJA
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein ametoa mwito kwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na Jeshi la Polisi nchini kuimarisha ulinzi katika eneo la pwani ya Mashariki ya kisiwa cha Unguja ambako shughuli nyingi za kitalii zinafanyika.
Alitoa mwito huo jana wakati alipozungumza na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba aliyemtembelea ofisini kwake Ikulu mjini Zanzibar.
“Umelieleza vyema suala la ulinzi wa pwani ya nchi yetu, lakini huku Zanzibar tuna biashara ya utalii na ukanda wa pwani ya Mashariki ambako kuna huduma nyingi za biashara hiyo uko wazi sana na ulinzi wake ni hafifu,” Dk Shein alimueleza waziri huyo.
Awali, Mwigulu alimueleza Rais Shein kuwa katika kipindi hiki na kijacho wizara yake inaelekeza suala la ulinzi wa pwani ya nchi kuwa la muhimu hasa ikizingatiwa suala la uendelezaji wa sekta ya gesi na mafuta katika ukanda wa pwani ya nchi yetu.
Katika hatua nyingine, Dk Shein alimueleza waziri huyo wasiwasi wake kuhusu kuongezeka kwa vifo vinavyotokana na ajali za barabani pamoja na vitendo vya rushwa vinavyofanywa na baadhi ya askari wa usalama barabarani ambavyo ni kinyume na maadili ya kazi zao.
Tuesday, October 4, 2016
URUSI YASITISHA MKATABA WA NYUKLIA BAINA YAKE NA MAREKANI
Mkataba baina ya Urusi na Marekani ambao unahusisha silaha za kinyuklia umesitishwa rasmi na nchi ya Urusi huku hali hiyo ikipelekea kuzorota kwa uhusiano baina ya nchi hizo mbili.
Urusi kupitia kwa Rais wake Vladimir Putin imesema imeamua kuchukua hatua hiyo ili kulinda usalama wa Urusi huku akiituhumu Marekani kwa kuunda vikwazo vyenye kutishia uthabiti kwa kuchukua hatua zisizo za kirafiki dhidi ya nchi yake.
Urusi pia imetoa masharti ambayo lazima yafuatwe na Marekani kabla ya kurejelewa kwa mkataba huo ambapo mwaka 2000 walikubaliana kila taifa kuangamiza tani 34 za madini ya Plutonium ambayo hutumika kutengeneza silaha za kinyuklia ambapo huo ulikuwa mpango wakimataifa wa kupunguza silaha za nyuklia duniani
Masharti iliyotoa Urusi kwa Marekani ni pamoja na kuitaka nchi hiyo kuondoa vikwazo vyote vilivyowekwa na nchi hiyo dhidi ya Urusi na kulipwa fidia iliyotokana na madhara yaliyojitokeza baada ya vikwazo hivyo. Pia imetaka Kupunguzwa kwa wanajeshi wa Marekani na silaha zake katika nchi zilizojiunga na Nato baada ya 1 Septemba 2000
Itakumbukwa Marekani pamoja na nchi za umoja wa ulaya waliiwekea Urusi vikwazo kufuatia hatua ya nchi hiyo kuchukua jimbo la Crimea kutoka kwa Ukraine mwaka 2014 pamoja na hatua ya nchi hiyo ya kuunga mkono wapiganaji wanaotaka kujitenga kwa maeneo ya mashariki mwa nchi ya Ukraine
Monday, October 3, 2016
NAPE- SIMBA WANATAKIWA KULIPA GHARAMA ZA UHARIBIFU WA VITI TAIFA
Serikali imezuia fedha za mapato ya mechi kati ya Simba dhidi ya Yanga hadi hapo gharama za uharibifu wa viti katika mechi yao dhidi ya Yanga, itakapojulikana.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amesema kwamba Simba inatakiwa kulipa gharama ya viti 1,781 vilivyoharibiwa na mashabiki wake.
Nape amesisitiza, fedha za mapato ya Simba zitaendelea kushikiliwa hadi hapo suala la gharama ya uharibifu itakapojulikana.
“Gharama ikijulikana, watakatwa mara moja. Na kama haitoshi, basi watalipishwa zaidi,” alisema.
Tayari kupitia Nape, serikali imetangaza kuzifungia Yanga na Simba kuutumia uwanja huo hadi hapo baadaye.
Mashabiki wa Simba waling’oa viti wakati wa mechi yao dhidi ya Yanga kwenye uwanja huo, jana ikiwa ni baada ya Amissi Tambwe kuifungia Yanga bao.
Tambwe raia wa Burundi, alifunga bao hilo baada ya kuunawa mpira, jambo ambalo lilisababisha tafrani hasa baada ya yeye kwenda kushangilia upande wa mashabiki wa Simba.
Saturday, October 1, 2016
KAMPENI YA MTIWANGU YAJA NA NEEMA HII ILALA
Ikiwa ni Octoba Mosi siku ambayo, imeshuhudiwa maeneo mbalimbali ya Jijini Dar es Salaam na Wilaya zake tano za Temeke, Ilala, Kinondoni, Ubungo na Kigamboni yakitekeleza agizo la Mkuu wa Mkoa huo Paul Makonda katika suala zima la upandaji wa Miti kupitia kampeni yake ya Mtiwangu.
Kampeni hiyo ambayo imezinduliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu, imeambatana na jambo lingine ambalo litawanufaisha wakazi wa Ilala na watanzania kwa ujumla.
Akizungumza juu ya suala hilo Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema ameelza kuwa kwa kushirikiana na kampuni ya mtandao wa simu ya TTCL wameweza kuweka ‘Internet’ ya bure kwa wakazi watakao kuwa wanaotembelea maeneo yenye bustani kubwa za mji, jambo litakalo wasaidia kupata taarifa mbalimbali zenye kuelimisha na kuwasiliana kupitia mitandao ya kijamii, ambapo Mkurugenzi wa TTCL Waziri Kindamba ameasema zoezi hilo halitakuwa la kusuasua kwani wamejipanga kufanya mapinduzi ya kimtandao na kuongeza kuwa Tanzania inakuwa nchi ya Tatu Afrika Mashariki kwa kufanya hivyo ikiungana na Kenya, Uganda, huku kwa Afrika ikiwa ya Tano zikiongezeka Nigeria na Afrika Kusini.
Kwa upande wake Makamu wa Rais amepongeza uwepo huo wa ‘Internet’ (WiFi) kwa maeneo yenye bustani ikiwemo NBC, Palm Beach, Mnazi Mmoja na Gymkana ambapo uzinduzi huo ulifanyika, huku akisisitiza suala la kutunza mazingira na upandaji miti liwe endelevu, kwani hali ya hewa ya Dar es Salaam imekuwa ya joto kutokana na athari za Mazingira, hivyo ameziagiza Wizara zinazosimamia Misitu na Mazingira kuzifuatilia bustani zote zilizopandwa miti siku ya leo.
MAGUFULI – JESHI LETU NI IMARA
RAIS John Magufuli amesema anaamini yuko salama kwa kuwa vyombo vya ulinzi na usalama nchini ni imara, vinaheshimika ndani na nje ya nchi na hakuna anayeweza kuichezea nchi.
Aidha ameagiza askari 40 wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na mgambo 30 walioshiriki kwenye zoezi la ‘Amphibious Landing’, kuajiriwa rasmi katika Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kuanzia leo, huku pia akitoa agizo la kutowapelekea fedha wafungwa katika Magereza yaliyoharibiwa na tetemeko la ardhi mkoani Kagera na badala yake wafungwa hao watumike kukarabati gereza hilo.
Hayo yalibainishwa mjini hapa jana na Rais Magufuli wakati akifunga rasmi mazoezi ya kutua ardhini kutoka majini, kukomboa eneo lililotekwa na adui (Amphibious Landing) ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya miaka 52 ya JWTZ.
Akizungumza baada ya zoezi la jeshi kukamilika, Rais Magufuli alisema ameridhika na kazi inayofanywa na jeshi hilo na kuwa hakuna mtu anayeweza kuichezea nchi.
“Tuna jeshi imara, linaloheshimika, sina mashaka, niko salama, chombo hiki ni nguzo muhimu ya amani nchini, ndio maana nataka linitumie kwa sababu lina nidhamu sana,” alisisitiza Rais Magufuli ambaye ni Amiri Jeshi Mkuu.
Thursday, September 29, 2016
RONALDO AUTAKA UMENEJA BAADA YA SOKA
Watu husema kuna maisha baada ya soka ama kitu husika ulichonacho lakini msemo huu hutumika kama kumkumbusha mtu afanye awezavyo ila anachokifanya kina mwisho, hivyo kama unafanya kazi ujue kuna siku lazima utaondoka ama hata ukiwa katika soka ipo siku utastaafu hivyo baada ya maisha hayo unaenda wapi ?.
Cristiano Ronaldo amesema kuwa anandoto za kuwa meneja wa soka baada ya kazi yake ya kucheza mpira. Nyota huyu pia umebaini katika mahojiano yake na kituo kimoja na ameweka wazi kuwa anaamini Klabu yake ya Real Madrid inaweza kufanya kitu kikubwa msimu huu haswa kuiga mafanikio ya ligi ya Mabingwa kama msimu uliopita.
Hii imekuja baada ya kushukuru uongozi wa soka aliowahi kupitia hivyo sio rahisi kwake kusahau kufundisha.
Tuesday, September 27, 2016
J.P.M KUZINDUA NDEGE MPYA KESHO
Pasi na shaka Ndege aina ya Bombardier Q400 zenye uwezo wa kubeba abiria 76 zilizotengenezwa nchini Canada ndio mkombozi sahihi kwa Watanzania kwani kwa kipindi kirefu sasa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) lilishindwa kujiendesha kutokana na sababu kadha wa kadha ikiwemo gharama za uendeshaji.
Moja ya sifa kuu ya ndege hii ni kuwa na uwezo wa kutumia mafuta kidogo, jambo litakalosaidia kupunguza gharama za usafiri huo wa ndege nchini kwa wasafiri wa ndani pamoja na kurahisisha mazingira ya uendeshaji; hadi sasa tayari zimekwisha wasili ndege mbili ambapo kesho zitazinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi) Dk. Leornard Chamuriho amesema maandalizi yote kwa ajili ya uzinduzi wa ndege hizo yamekamilika na uzinduzi huo utafanyika kesho kuanzia saa mbili asubuhi.
“Tunawaomba wanahabari na wananchi kujitokeza kwa wingi katika uzinduzi huo ili waone utekelezaji wa ahadi za serikali katika mkakati wa kuhuisha usafiri wa anga hapa nchini”, amesema Dk. Chamuriho.
Monday, September 26, 2016
FIESTA 2016 MOSHI (+Pichaz)
Ule msimu wa burudani ya Tigo Fiesta inayopita mkoa hadi mkoa kukamilisha orodha ya mikoa 15 ambayo Tamasha la Fiesta litapita, jana katika Viwanja vya Majengo Moshi ilikuwa zamu ya wakazi wa mji huo na mikoa ya jirani kufurahia utamu wa Tigo Fiesta 2016.
Sheta akifanya yake jukwaani katika Tigo Fiesta Moshi
Kwa kifupi Fiesta ni burudani ambayo pia inakuwa na fursa kadha wa kadha huku ikiacha historia iliyotukuka kila inapopita. Jicho la Mtembezi lilikuwepo katika burudani ya Tigo Fiesta ambapo mastaa hawa walifanya yao katika jukwaa la Fiesta Moshi.
Mkali wa Hip Hop Darasa nae hakuwa nyuma alikunukisha ile mbaya
Byser maarufu kama Mr. Blue akikonga nyoyo za mashabiki katika jukwaa la Tigo Fiesta Moshi
Mamong’oo a.k.a manjeree machalii ya R wakifanya yao jukwaani usiku wa jana pale Viwanja vya Majengo Moshi
Mkali kutoka Manzese Tip Top Connection Madee akifanya makamuzi Tigo Fiesta Moshi
Snura Mushi mamaa wa majanga akishindua katika jukwaa la Tigo Fiesta Moshi
Hamadai mzigoni akiangusha burudani ya nguvu kwa Wanamoshi
Saturday, September 24, 2016
BEYONCE NA RIHANNA MFANO TOSHA KWA WASANII BONGO
Kama ilivyo kawaida ya bidhaa yenye matangazo mengi ndio itakayomalizika dukani kwa kununuliwa kwa wingi, ila linapokuja suala zima la kutengeneza kiki umuhimu wa kujua kuitumia unatakiwa kwa kiasi kikubwa kwa sababu ukikosea sehemu ndogo tu utakuwa umeingia kwenye kashfa ambazo hazitakuletea faida yoyote.
Msanii Beyonce aliwahi kutengeneza picha iliyowafanya ulimwengu mzima uamini kuwa yeye na mumewe ambaye ni mwanamuziki mkubwa wa miondoko ya Hiphop Jay Z, wanataka kuachana kutokana na mwanaume kukosa uaminifu katika ndoa yao, lakini mpaka inakuja kugundulika kuwa ilikuwa ni kiki ya album ya Lemonade wawili hao walikuwa wameshatengeneza pesa za kutosha kwa kuuza album hiyo.
Hili linaonekana kujirudia kwa msanii Rihanna ambaye aliwaaminisha wengi kuwa ana mahusiano ya kimapenzi na msanii Drake lakini kuna uwezekano mkubwa ikawa ni kiki ya kuuza albumu yake ya Anti, kwa maana hata zile tatoo ni kwa ajili ya kutengeneza pesa kwa mauzo ya albam.
Thursday, September 22, 2016
BARAKA DA PRINCE NA SABABU ZA NISAMEHE KUWA ‘HITSONG’ (Audio)
MTV MAMA 2016 MWAKA WA DIAMOND, KIBA NA NAVY KENZO
Hatimaye vipengele vya Tuzo za MTV Mama kwa mwaka 2016 vimewekwa hadharani huku wasanii 3 kutoka Tanzania wakitangazwa kuwania tuzo hizo katika baadhi ya vipengele. Katika vipengele hivyo vipatavyo 8 nchi ya Tanzania inawakilishwa na wasanii Diamond Platnumz, Ali Kiba pamoja na Kundi la Navy Kenzo.
Tuzo hizo zenye heshima kubwa sana barani Afrika zinatarajiwa kufanyika nchini Afrika Kusini Jumamosi ya Oktoba 22 mwaka huu zikiwahusisha pia wasanii nyota wa ndani na nje ya Afrika kuchuana kutwaa tuzo hizo.
Diamond Platnumz ambaye anashiriki kwa mara ya nne mwaka huu akifanya hivyo mwaka 2010 alipokuwa kwenye vipengele 2, ‘best new artist’ na ‘best male’ lakini hakufanikiwa kuchukua tuzo, mwaka 2014 tena alifanikiwa kuchaguliwa kwenye tuzo hizi wakati huo akiwa kwenye kipengele kimoja tu cha ‘best collaboration’ kwenye wimbo wa ‘my number one remix’ alioshirikiana na Davido hata hivyo haukuweza kunyakua tuzo hiyo. Mwaka 2015 ulikuwa wa bahati sana kwake mara baada ya kunyakua tuzo moja kati ya alizokuwa akiwania, akiwekwa kwenye vipengele 3 ‘best male’ ‘best collaboration’ na ‘best live act’ ambacho kilimpa tuzo. Mwaka huu yupo katika kipengele kimoja tu cha ‘best male’ ambapo anagombea tuzo hizi na wakali kibao kama, Black Coffee wa South Africa, AKA wa South Africa, Wiz Kid pamoja na Patoranking wote wa Nigeria.
Wawakilishi wengine wa Tanzania katika tuzo hizi, ni kundi la Navy Kenzo wenyewe hii ni mara yao ya kwanza kuingia kwenye tuzo hizi lakini wakichagizwa na vibao vyao vilivyofanya vizuri sana kwenye bara la Afrika kama ‘game’ walioshirikiana na Vanessa Mdee pamoja na ‘Kamatia’ ambao umefanya vizuri sana kwenye vituo mbalimbali vya radio na tv barani Afrika wapo tayari kupambana kwenye kipengele cha ‘best group’ ambapo watachuana vikali na makundi mengine kama ‘Toofan’ kutoka Togo, ‘Micasa’ South Africa pamoja na ‘R2Bees’ kutoka Ghana.
Ali Kiba ni msanii mwingine kutoka Tanzania ambaye licha ya kupata nafasi ya kutumbuiza kwenye tamasha hilo, pia atawania tuzo ya wimbo bora wa kushirikiana ‘best collaboration’ kupitia wimbo alioshirikishwa na kundi la Sauti Sol uitwao ‘Unconditionally Bae’.
Ni wakati wa Watanzania sasa kuwapa sapoti wasanii wetu hawa kwa kuwapigia kura kwa wingi ili watuwakilishe vyema kwa kuleta tuzo hizi nyumbani.
Subscribe to:
Posts (Atom)




















































