Monday, October 10, 2016

JPM- WATANZANIA WAFICHUENI WAVURUGA AMANI


RAIS John Magufuli amewataka watanzania kuwa mstari wa mbele, kutunza amani yao kwa kuhakikisha wanawafichua wale wote wenye lengo ya kuivuruga amani hiyo.

Pia, ametoa changamoto kwa vyombo vya habari nchini kuweka zaidi uzalendo mbele na kuandika habari za maendeleo ya nchi zinazoonekana, badala ya kung’ang’ania kuandika habari zenye mlengo wa kuiponda serikali pekee.

Rais alisema hayo mwishoni mwa wiki, wakati akizindua kiwanda cha kusindika matunda kinachomilikiwa na kampuni ya Food Products ya Bakhresa kilichopo katika Kijiji cha Mwandege wilayani Mkuranga mkoani Pwani.


Alisema endapo Watanzania wataichezea amani iliyopo iliyodumu kwa muda mrefu, jitihada za serikali za kuijenga nchi kiuchumi na kimaendeleo ikiwemo uchumi wa viwanda, kamwe hazitazaa matunda.

“Navipongeza vyombo vya dola kwa jitihada zake za kuhakikisha nchi inadumu kwenye amani, nawahakikishia serikali haitovumilia mtu yeyote mwenye nia ya kuivuruga amani hii,” alisisitiza.

Alifafanua kuwa Tanzania ni moja kati ya nchi zinazozungumziwa kuwa uchumi wake kuwa unakua kwa kasi barani Afrika; huku uchumi wake katika robo ya pili ya mwaka pekee ukifikia asilimia 7.9.

“Lengo la serikali yangu ni kuhakikisha uchumi unakua na kufikia asilimia 7.2 lakini hadi robo ya pili ya mwaka tumefikia asilimia 7.9 tumevuka lengo. Hii ina maana kuwa mpaka tufikie robo tatu hata kama hapo katikati kutatokea mgogoro kidogo wa kiuchumi tutaweza kufikia lengo la asilimia 7.2,” alisema.



Jiunge na hatukwamii.blogspot.com/ sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video 


0 comments:

Post a Comment