Monday, October 10, 2016

Matani ya Stan Bakora yamtoa povu Barakah The Prince

Mchekeshaji Stan Bokora baada ya kufanya cover ya wimbo ‘Nisamehe’ wa Barakah Da Prince kumezuka mtafaruku baina ya wawili hao.


Baada ya mchekeshaji Stan Bakora kuirudia ngoma ya Baraka The Prince, mdundo wa ‘Nisamehe‘, Baraka ameiona video yenyewe na imeonekana hajapendezwa na ndio maana kwenye Instagram kaamua kumpa Stan Bakora onyo.


Kwa upande wa Stan Bakora alisema kila video ambayo anafanya cover ni lazima azungumze kwanza na mwenye kazi na kukubaliana naye.

Maneno ya Baraka The Prince ‘Matani ni mazuri ila yakizidi yanaweza kuleta matatizo… heshima ichukue nafasi yake tafadhali mzee utani huu sijaupenda iwe mwanzo na mwisho tafadhali


Jiunge na hatukwamii.blogspot.com/ sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video 


0 comments:

Post a Comment