Saturday, October 8, 2016

Rais Dkt. Magufuli apongeza dhehebu la Bohora kwa kuadhimisha siku ya mwaka mpya wa kiislamu nchini

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John pombe Magufuli akisalimiana na Kiongozi wa Jumuiya ya Mabohora Duniani, Dk Seydna Mufaddal Saifuddin mara alipowasili kwenye msikiti wa Bohora ulioko Upanga jijini Dar es salaam  ambako alikuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za Mabohora kuadhimisha Mwaka Mpya wa Kiislamu wa 1438 leo Oktoba 8, 2016

Ambapo amepata fursa ya kuwahutubia katika tamasha la madhehebu ya Bohora ambayo yanafanya maadhimisho ya dunia ya sikukuu ya mwaka mpya wa Kiislam yanayoendelea Jijini Dar es Salaam.
Maadhimisho hayo yamewaleta nchini wafuasi zaidi ya 30,000 kutoka nchi mbalimbali duniani na kuongozwa na Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Bohora Duniani Mtukufu Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin Saheb (TUS).
Akihutubia wafuasi wa Bohora katika Msikiti wa Hakimi uliopo Upanga Jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli amemshukuru Kiongozi Mkuu wa Bohora kwa kukubali kufanya maadhimisho ya mwaka mpya wa madhehebu hayo hapa nchini na amewashukuru na kuwapongeza wafuasi wa madhehebu hayo kwa kukubali kuja hapa nchini na kukaa kwa siku zote za maadhimisho yaani kuanzia tarehe 02 Oktoba, 2016 walipoanza hadi tarehe 11 Oktoba, 2016 watakapomaliza.
Rais Magufuli, amewapongeza viongozi na wafuasi wa madhehebu ya Bohora kwa kutumia maadhimisho haya kuhimiza amani, upendo na mshikamano na pia amewashukuru kwa kushiriki katika
maendeleo ya kijamii na kiuchumi ikiwemo mchango Dola za Marekani 53,000 zilizotolewa na Kiongozi Mkuu wa Bohora kwa Serikali kwa ajili ya kuchangia kampeni ya utengenezaji wa madawati, na kuwaleta madaktari kutoka Hospitali ya Saifee ya India waliotoa matibabu bure kwa wananchi wa Arusha.
Aidha, Rais Magufuli amewakaribisha wafuasi wa Bohora duniani kuja kuwekeza hapa nchini
katika sekta mbalimbali zikiwemo Kilimo, Uvuvi, Misitu, Mifugo, Madini na Gesi kwani soko la uhakika lipo ndani ya nchi, katika Jumuiya ya Afrika Mashariki na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) yenye watu takribani milioni 400.
Kwa upande wake Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Bohora Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin Saheb (TUS) amemshukuru Rais Magufuli kwa kuungana na wafuasi wa madhehebu ya Bohora katika
maadhimisho hayo na amesema wafuasi wote wa Bohora wanahimizwa kushirikiana na mamlaka zilizopo katika nchi wanazoishi, kuwa raia wema na kufuata sheria.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia katika tamasha la madhehebu ya Bohora leo Oktoba 08, 2016, ambayo yanafanya maadhimisho ya dunia ya sikukuu ya mwaka mpya wa Kiislam Jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John pombe Magufuli akiagana   Kiongozi wa Jumuiya ya Mabohora Duniani, Dk Seydna Mufaddal Saifuddin kwenye msikiti wa Bohora ulioko Upanga jijini Dar es salaam ambako alikuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za Mabohora kuadhimisha Mwaka Mpya wa Kiislamu wa 1438 leo
Sehemu ya waumini kinababa kwenye msikiti wa Bohora ulioko Upanga jijini Dar es salaam   sherehe za Mabohora kuadhimisha Mwaka Mpya wa Kiislamu wa 1438 leo 


sehemu ya waumini kinamama na watoto kwenye msikiti wa Bohora ulioko Upanga jijini Dar es salaam   sherehe za Mabohora kuadhimisha Mwaka Mpya wa Kiislamu wa 1438 



Jiunge na hatukwamii.blogspot.com/ sasa


Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video 



0 comments:

Post a Comment