Showing posts with label dewjiblog. Show all posts
Showing posts with label dewjiblog. Show all posts

Friday, October 14, 2016

Tanzania yaongoza ukuaji wa Uchumi Afrika- Waziri Mkuu Majaliwa



WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Tanzania ni miongoni mwa nchi saba Barani Afrika ambazo uchumi wake unakua kwa kasi zaidi hivyo amewakaribisha wawekezaji kuja kuwekeza kwenye sekta mbalimbali ikiwemo ya viwanda.
Tanzania ni nchi ya pili kwa kasi ya ukuaji wa uchumi Barani Afrika ambapo uchumi wake unakuwa kwa asilimia 7 ikiongozwa na Ivory Coast inayokua kwa asilimia 8.5, Senegal ya tatu (asilimia 6.6), D’jibout ya nne (asilimia 6.5), Rwanda ya tano (asilimia 6.3), Kenya ya sita (asilimia 6.0) na Msumbiji ya saba (asilimia 6.0).
Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo jana jioni (Alhamis, Oktoba 13, 2016) wakati akifungua kongamano la Jumuiya ya Dawoodi Bohora lililohusu fursa za uwekezaji.
Amewakaribisha wanajumuia hiyo kuja kuwekeza nchini. Kongamano hilo lilifanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwalimu Nyerere.
“Tanzania ina sera nzuri za kiuchumi ambazo zimesababisha uchumi wake kuendelea kuwa imara kwa zaidi ya miongo miwili sasa. Naikaribisha jumuiya ya Bohora kuja kuwekeza na kufanya biashara Tanzania,” alisema.
Waziri Mkuu alisema makampuni yatakayowekeza nchini yatafaidika na uwepo wa malighafi za kutosha, sera nzuri uwekezaji pamoja na uhakika wa usalama wa mali zitakazowekezwa nchini kwa sababu ya hali ya amani na utulivu iliyoko nchini.

Alisema licha ya Tanzania kuwa maeneo mazuri kwa ajili ya uwekezaji pia ina soko la uhakika kwa sababu ya kuwa mwanachama wa jumuiya mbili ambazo ni Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) zenye watu takriban milioni 600.
“Tanzania ni kitovu cha biashara kwani inapakana na nchi nane ambazo kati yake nchi sita zinatumia bandari ya Dar es Salaam kusafirisha mizigo yake. Mizigo hiyo husafirishwa kwa njia ya reli na barabara,” alisema.
Nchi zinazopakana na Tanzania ni Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Malawi, Zambia, Msumbiji, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC). Zinazotumia bandari ya Dar es Salaam ni Uganda, DRC, Rwanda, Burundi, Malawi na Zambia.
Kwa upande wake Mratibu wa Kongamano hilo la kidini (Ashara Mubarak) lililowakutanisha Mabohora kutoka duniani kote Bw. Murtaza Adamjee ameahidi kushirikiana na Serikali katika kutangaza fursa za uwekezaji zilizoko nchini.
Bw. Adamjee alimuhakikishia Waziri Mkuu kwamba Mabora dunia nzima wanakuja Tanzania kuwekeza katika sekta mbalimbali hususan ya viwanda. “Tutafikisha ujumbe kwa Mabohora dunia kote kwamba Tanzania ni sehemu salama ya kuja kuwekeza,”

Jiunge na hatukwamii.blogspot.com/ sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video 



Kamanda Choughule:”Vijana tumuenzi Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere kwa kufanya kazi


Mwenyekiti wa CCM, Shina la Pamba Road, Dar es Saaam, Sharik Choughule, amewaasa vijana kumuenzi Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere kwa kufanya kazi za kujiajiri.
Amesema, kufanya hivyo kutawawezesha vjana wengi kuwa na ajira za uhakika, badala ya kusubiri ajira za serikali au taasisi mbalimbali kwa kuwa nafasi za ajira katika sekta hizo ni chache huku mahitaji yakiwa ni makubwa.
Choughule ambaye pia ni Kamanda wa Vijana Kata ya Kivukoni, Dar es Salaam, amesema hayo leo wakati akizungumzia kumbukumbu ya miaka 17 ya Kifo cha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, ambayo Maadhimisho yake yanafayika leo Kitaifa mkoani Simiyu kwa shughuli ya kuzima Mwenge.
Amesema, ili kuweza kufanya kazi za kujiajiri, vijana ni lazima kwanza kuondoa woga, ili kujiamini kuwa wanaweza kwa kuwa ajira binafsi zipo nyingi hasa ikizingatiwa kwamba wengi siku hizi wana elimu za kutosha hadi za viwango vya Chuo Kikuu.
“Vijana lazima tujiamini kwa kuwa sisi ndiyo tegemeo la taifa, hivyo siyo busara vijana kuanza kulalamika kuwa hatuna ajira kwa lengo la kutarajia kuwa Taifa ndilo tulitegemee kutupatia ajira, hayo si mawazo mwafaka kwa afya ya nchi yetu”, alisema Shoughule.
Sharik Choughule

Alisema, hatua ya vijana kuanza kuweka kisingizio cha ukosefu wa ajira za kuajiriwa, kinawadumaza vijana na kukosa maamuzi ya kubuni au kukosa ubunifu wa kubuni miradi aina tofauti tofauti kwa manufaa yao.
Choughule alisema, hivi sasa umefikia wakati wa vijana kuachana na mawazo mgando, kwa wasababu baadhi ya vijana ambao wameonyesha uthubutu, wameweza kujiajiri katika sekta za mitandao ya mawasiliano ambayo ni sekta imeenea duniani kote.
Alisema, mfano mzuri wa kuigwa ni vijana walipo Jeshi la Kujenga Taifa, JKT, ambao wamekuwa wakionyesha kufanya kazi nyingi ambazo siyo za kuajiriwa ikiwemo kuanzisha shughuli za kilimo cha kisasa, ufugaji na ufundi wa aina mbalimbali ikiwemo kutengeneza samani na ujenzi wa nyumba.
Choghule amesema, hatua ya vijana kufanyakazi za kujiajiri siyo tu watakuwa wamemuenzi Baba wa taaifa Mwalimu Nyerere, lakini pia watakuwa wamemuunga mkono Rais Dk John Magufuli katika azma yake ya kukuza uchumi wa taifa kwa kaulimbiu yake ya ‘Hapa kazi tu’.

Jiunge na hatukwamii.blogspot.com/ sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video 





Ujumbe wa Mama Janeth Magufuli katika siku ya kumbukumbu ya kifo cha Mwl. Nyerere


Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli amewataka watanzania kumuenzi kwa vitendo Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa kuwahudumia Wazee nchini kwa kuwapatia mahitaji ya muhimu kwa ajili ya ustawi wa maisha yao.
Akiongea na Wazee katika Kambi ya kulea wazee ya Chazi iliyopo Wilayani Mvomero Mkoani Morogoro Mama Janeth amesema kuwa watanzania wanapaswa kutambua Wazee ni kundi muhimu kwa ustawi wa nchi kwani miongoni mwao walishiriki katika ukombozi wa taifa leo hivyo tuitumie Siku kama ya leo na nyingine kumuenzi Hayati mwalimu Julius Nyerere akiwa kama mzee aliyetangulia mbele za haki.
“Leo ni siku muhimu sana katika taifa letu siku ambayo tunaenzi siku aliyofariki muasisi awa Taifa letu Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, hivyo ni rai yangu kwa watanzania kwa ujumla kumuenzi kwa kushiriki kwa pamoja katika kuwahudumia wazee na kuwapatia mahitaji yao muhimu” Alisema Mama Janeth.
Aidha, Mama Janeth alisema kuwa amesikia changamoto zinazokabili Makazi hayo na ameahidi kuendelea kushirikiana na wadau kwa kadri iwezekanavyo ili kuhakikisha wanapunguza na kuondoa kabisa changamoto hizo iwe makazi ya wazee Chazi na yote nchini yawe sehemu salama ya kuwahudumia wazee.
Katika kutembelea kituo hicho Mamam Janeth Magufuli ametoa zawadi ya mchele, Maharagwe,unga na mafuta ya kupikia kwa ajili ya wazee na watu wasiojiwezakatika kituo hicho.
Akimkaribisha Mgeni Rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Stephen Kebwe amesema kuwa serikali ya mkoa wake inatekeleza kwa vitendo maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. john Pombe Magufuli ya kuwahudumia wazee na kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ndani mkoa wameshaanza kutatua baadhi ya kero na wataendelea kufanya hivyo ili kuyaimarisha makazi ya wazee mkoani humo.
Pia Dkt. Kebwe amewataka watu wote waliovamia makazi ya wazee kuondoka mara moja na kutafuta maeneo mengine na atakayekiuka agizo hilo serikali itamchukulia hatua kali za kisheria.
Akiwasilisha Risala ya Makazi ya Ya wazee ya Chazi kwa Mama Janeth Magufuli Kaimu Afisa Mfawidhi wa Makazi hayo Bw. Richard Kamwana amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa misaada aliyoitoa kwa wazee wa kituo hicho wakati wa sikukuu ya Eid.
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero Bw. Florent Kiombo amemuhakikishia Mama Janeth Magufuli wataendelea kushirikiana na taasisi nyingine katika kukiendeleza kituo hicho ikiwamo kuwapatia wazee wote kadi za CHF kwa ajili ya kuwasaidia wazee hao kupata huduma ya Afya popote waendapo.
Na Hassan Silayo-MAELEZO

Jiunge na hatukwamii.blogspot.com/ sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video 



Mfalme wa Morocco kufanya ziara nchini Tanzania


Mfalme Mohammed wa VI wa Morocco anatarajiwa kufanya ziara rasmi nchini kuanzia tarehe 19 hadi 23 Oktoba, 2016.
Madhumuni ya ziara hiyo ni kukuza zaidi uhusiano kati ya Tanzania na Morocco hususan katika masuala ya kiuchumi na kibiashara kwa faida ya nchi hizi mbili na watu wake.
Vilevile, Mfalme Mohammed wa VI wa Morocco atatumia fursa ya ziara hiyo kutembelea Zanzibar na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kwa ajili ya kujionea vivutio vya utalii vilivyopo nchini.
Hata hivyo, ziara hiyo ambayo imejikita zaidi katika kukuza ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara haitaathiri msimamo wa Tanzania katika mgogoro unaoendelea kati ya Morocco na Sahara Magharibi.

Msimamo wa Tanzania ambao umekuwa ukisimamiwa na Awamu zote za uongozi zilizopita na Awamu hii, upo sambasamba na ule wa Umoja wa Afrika (AU) unaoutaka Umoja wa Mataifa (UN) ambao ndio wamepewa jukumu la kusimamia mgogoro huo, kuongeza kasi katika kuutatua na kupata suluhu ya kudumu ya mgogoro huo.
Tarehe 20 Oktoba, 2016 Mhe. Mfalme Mohammed wa VI atakutana kwa mazungumzo ya faragha na Mhe. Rais Magufuli Ikulu yakifuatiwa na mazungumzo rasmi kati yao na wajumbe waliofuatana nao.
Mhe. Mfalme Mohammed VI pamoja na kutembelea Tanzania, pia atatembelea Rwanda, Ethiopia na Kenya.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Dar es Salaam.

Jiunge na hatukwamii.blogspot.com/ sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video 





Thursday, October 13, 2016

ZANZIBAR yaadhimisha siku ya Uoni Duniani

Mtaalamu wa macho kutoka China Dkt. Zhao Wei akimpima macho Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo kwenye maadhimisho ya siku ya uoni Duniani yaliyofanyika kitaifa kituo cha Afya cha Magogoni, Mjini Zanzibar.

Waziri wa Afya Visiwani Zanzibar, Mh. Mahmoud Thabit Kombo amewataka wananchi kuendelea kuvitumia vituo vya  afya vilivyo  karibu  nao vinavyotoa huduma  za macho katika jamii ili kupambana na upofu usiowalazima.
Amesema vituo vingi vya Afya hivi sasa vimewekewa huduma muhimu za uchunguzi wa maradhi mbali mbali, ikiwemo uchunguzi wa macho, na hakuna haja ya wananchi kukimbilia Hospitali Kuu ya Mnazimmoja.
Waziri Mahmoud ameeleza hayo katika maadhimisho ya siku ya uoni Dunini yaliyofanyika Kitaifa kituo cha Afya Magogoni Wilaya ya Magharibi B.
Amesema  madaktari wanapohisi tatizo ni kubwa na haiwezekani kupata matibabu katika vituo vidogo wanaamua kumpeleka mgonjwa Hospitali Kuu hivyo hakuna haja ya kuwa na wasiwasi na viituo hivyo.
Amesema tatizo la uoni limekuwa kubwa duniani kote na inakisiwa hivi sasa  kuna watu wasioona wapatao milioni 285 na asilimia 37 kati yao hawaoni kabisa.
Kwa upande wa Zanzibar amesema inakisiwa kuwa na watu 10,000 ambao wanamatatizo ya uoni na asilimia 50 kati ya hao hawaoni kabisa kutokana na sababu mbali mbali.
Waziri wa Afya ameongeza kuwa wataalamu wa maradhi ya tiba ya macho nchini kwa kushirikiana na Shirika la Afya ulimwenguni (WHO) pamoja na taasisi mbali mbali duniiani wako katika mikakati ya kutafuta ufumbuzi wa matatizo ya maradhi ya macho.
Hata hivyo amesisitiza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara ya Afya inajitahidi kuendeleza huduma za matibabu ya macho katika nyanja zote katika vijiji mbali mbali Unguja na Pemba kupitia Kitengo chake cha Afya ya msingi ya matibabu ya macho vijijini.
Amewataka wananchi kufanya juhudi kuepuka maradhi ambayo yanapelekea matatizo ya macho na kujenga utamaduni wa kufanya mazoezi mara kwa mara kwani ni moja ya tiba ya kujiepusha na maradhi mengi.
Aidha alilishukuru Shirika la Kimataifa la Sightsaver kwa ushirikiano wake wa karibu na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na misaada ya kitaalamu na dawa wanazosaidia kitengo cha matibabu ya macho.
Katika risala ya wafanyakazi wa Kitengo cha matibabu ya macho iliyosomwa na Mratibu wa Kitengo hicho Dkt. Rajab Mohammed Hilal wamesema wanakabiliwa na udogo wa nafasi ya kutekeleza katika kitengo hicho.
Mratibu wa huduma za macho Zanzibar Dkt. Rajab Mohammed Hilal akisoma risala ya kitego cha matibabu ya macho kwenye maadhimisho ya siku ya uoni Duniani yaliyofanyika Kituo cha Afya Magogoni, Mjini Zanzibar.
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kupima macho kwenye maadhimisho ya siku ya uoni Duniani yaliyofanyika Kituo cha Afya Magogoni wakiendelea kuangaliwa macho.


Jiunge na hatukwamii.blogspot.com/ sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video 
Thabiti Kombo



Majambazi waliouwa askari Polisi Mbande walioua, mmoja asakwa


Kikosi Maalumu cha Kupambana na Ujambazi wa Kutumia Silaha cha Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kilifanikiwa kukamata watuhumiwa wanne wa ujambazi waliohusika katika mauaji ya askari polisi 4 katika benki ya CRDB iliyopo maeneo ya Mbande, Mbagala jijini Dar es Salaam.
Kamishna wa Kanda hiyo, Kamanda Simon Sirro wakati akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, amesema watuhumiwa hao walikamatwa wakati wa majibizano ya risasi yaliyotokea Oktoba 11, 2016 katika pori la Dondwe lililopo Chanika.
“Kikosi kilifanikiwa kumkamata mtuhumiwa mmoja, baada ya kupata taarifa kutoka kwa raia wema kuwa ni jambazi na ndiye aliyehusika katika mauaji ya askari polisi huko Mbande,” amesema.
Kamanda Sirro ameongeza kuwa “Baada ya kumkamata mtuhumiwa huyo alikiri kuhusika na tukio hilo akiwa na wenzie saba, alitupeleka mahala walipo wenzake, ila alikimbia, wenzie walipojua polisi wapo maeneo hayo, walianza kurusha risasi ndipo polisi nao wakaanza kurusha risasi.”
Kamanda Sirro amesema kuwa, watuhumiwa hao walizidiwa na mashambulizi ya risasi ambapo walijeruhiwa vibaya na kwamba walifariki dunia wakiwa wanapatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Amesema askari polisi walifanikiwa kuipata bunduki ya kijeshi aina ya SMG iliyofutwa usajili ambayo watuhumiwa hao waliipora kutoka mikononi mwa polisi waliowaua mbande ikiwa na risasi 22 ndani ya magazine.
Katika tukio lingine, Kamanda Sirro amesema mnamo Oktoba 11, 2016 maeneo ya magomeni polisi wakiwa doria walifanikiwa kukamata bastola moja aina ya bereta baada ya kutelekezwa na kundi la vijana.
Pia amesema Jeshi la Polisi limekamata watuhumiwa watatu wakiwa na bomu moja la kienyeji, mapanga manne, visu viwili, na bisibisi moja.
Vilevile Jeshi la Polisi Dar es Salaam Oktoba 12, 2016 walikamata panya road zaidi ya 10 maeneo ya Mbagala.

Jiunge na hatukwamii.blogspot.com/ sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video 




Trey Songz asababisha Jux kumfollow Vee Money Instagram, Jux afunguka


Kufuatia kusambaa picha katika mitandao ya kijamii ikimwonyesha staa wa muziki wa Marekani, Trey Songz akiwa na Vanessa Mdee kisha mpenzi wa Vee Money, Jux kumfollow Vanessa Instagram, staa huyo wa muziki nchini amefunguka sababu ya kufanya jambo hilo ambalo kwa kipindi chote ambacho amekuwa na Vanessa alikuwa hajakifanya.
Akiwa katika kipindi cha XXL cha Clouds Fm, Jux alisema alifikia uamuzi wa kumfollow Vanessa ili kupunguza maneno kutoka kwa mashabiki wao ambao walikuwa wanahisi kuwa yawezekana wapendanao hao watakuwa wamegombana kutokana na picha ya Vee Monney na Trey Songz.
“Kuna mambo watu wanaamini lakini mimi mtu asiponipost hata Istagram siwezi kummind, mimi sijawahi kumfollow [Vanessa] na yeye hajawahi, sio kitu muhimu sana maana tunaongea mara nyingi zaidi, Instagram tunachukulia ni zaidi ya maisha ya watu,
“Kwakuwa nilikuwa sijamfollow nikaona nimfollow sababu ya mambo yaliyotokea ili watu waone hakuna ishu, baada ya kutokea yale ilikuwa inamsumbua huyu na mimi nipo mbali hata akipiga naweza kuwa nimelala sababu tunapisha muda kule [China] na huku, mimi bado sana kummind ni mtoto wa kike lazima nimpe sapoti,” alisema Jux na kuongeza.
“Mimi ni mtu ambaye namsapoti sana, na mimi nilikuwa namwambia unaenda Coca Studio ajaribu kutafuta nafasi ya kuongea na menejimenti zao wasanii ambao atakutana nao ili kama kuna uwezekano wa kufanya kazi afanye”

Jiunge na hatukwamii.blogspot.com/ sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video