Kufuatia kusambaa picha katika mitandao ya kijamii ikimwonyesha staa wa muziki wa Marekani, Trey Songz akiwa na Vanessa Mdee kisha mpenzi wa Vee Money, Jux kumfollow Vanessa Instagram, staa huyo wa muziki nchini amefunguka sababu ya kufanya jambo hilo ambalo kwa kipindi chote ambacho amekuwa na Vanessa alikuwa hajakifanya.
Akiwa katika kipindi cha XXL cha Clouds Fm, Jux alisema alifikia uamuzi wa kumfollow Vanessa ili kupunguza maneno kutoka kwa mashabiki wao ambao walikuwa wanahisi kuwa yawezekana wapendanao hao watakuwa wamegombana kutokana na picha ya Vee Monney na Trey Songz.
“Kuna mambo watu wanaamini lakini mimi mtu asiponipost hata Istagram siwezi kummind, mimi sijawahi kumfollow [Vanessa] na yeye hajawahi, sio kitu muhimu sana maana tunaongea mara nyingi zaidi, Instagram tunachukulia ni zaidi ya maisha ya watu,
“Kwakuwa nilikuwa sijamfollow nikaona nimfollow sababu ya mambo yaliyotokea ili watu waone hakuna ishu, baada ya kutokea yale ilikuwa inamsumbua huyu na mimi nipo mbali hata akipiga naweza kuwa nimelala sababu tunapisha muda kule [China] na huku, mimi bado sana kummind ni mtoto wa kike lazima nimpe sapoti,” alisema Jux na kuongeza.
“Mimi ni mtu ambaye namsapoti sana, na mimi nilikuwa namwambia unaenda Coca Studio ajaribu kutafuta nafasi ya kuongea na menejimenti zao wasanii ambao atakutana nao ili kama kuna uwezekano wa kufanya kazi afanye”
Jiunge na hatukwamii.blogspot.com/ sasa
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video
0 comments:
Post a Comment