Baada ya kumalizika mchezo wa VPL kwa Mbeya City kupata kichapo cha goli mbili kwa bila kutoka kwa Simba, uongozi wa klabu hiyo umesema kuwa umepokea matokeo hayo na kukubali kuwa wamefungwa kwa uwezo na Simba.
Hayo yamesemwa na Msemaji wa Mbeya City, Dismas Temu na kusema kuwa ni hali ya kawaida katika mchezo kupata matokeo mazuri au kupata matokeo mabaya na hivyo wanakubaliana na matokeo kwani wapinzani wao walitumia vizuri nafasi walizozipata.
“Ni kawaida kupoteza mchezo, ni kawaida kufungwa ni kawaida kushinda huu ni mchezo wa makosa, hatujajichanganya ni swala tu la mchezo wa soka, timu yetu imecheza vizuri, swala la nafasi nani anatumia nani hatumii ni jambo lingine,
“Simba wametengeneza nafasi chache na wamefanikiwa kuzitumia, na sisi tumetengeneza na tumeshindwa kuzitumia, hayo ndiyo matokeo na nadhani ni jambo zuri kukubaliana na matokeo,” alisema Temu.
0 comments:
Post a Comment