Thursday, September 29, 2016

SONY WAMEMLEGEZEA KAMBA DAVIDO, AACHIA COVER YA ALBUM YAKE MPYA


Hatimaye Sony wameamua kuachia album mpya ya Davido baada ya kukaa kimya kwa miezi tisa tangu ajiunge na label hiyo mapema mwaka huu.
Album hiyo ambayo imekuwa ikihairishwa mara nyingi inaonekana itatoka hivi karibuni, Davido ametoa tangazo lililosubiriwa kwa muda mrefu na mashabiki wake, kuanzia tarehe 30 mwezi huu album hiyo itakuwa tayari kwa ajili ya kupre-order.
Wiki chache zilizopita Davido aliamua kutoa malalamiko yake kwa label hiyo baada ya kusogeza mbele tarehe ya kuachia video yake mpya aliyomshirikisha Tinashe.

0 comments:

Post a Comment