Asubuhi ya leo katika kipindi cha Leo Tena cha Clouds Fm alikuwepo kijana Said, kijana ambaye tukio alilofanyiwa limewagusa wengi baada ya kutobolewa macho na kijana ajulikanae kama Scorpion.
Ni katika kuendeleza kampeni ya kumuombea mchango kijana huyo kwa yeyote aliyeguswa na tukio hilo ili kuhakikisha kijana Said anapata matibabu na kurudi katika hali yake ya kawaida kama itawezekana.
Diamond Platnumz ni mmoja kati ya walioguswa vilivyo na tukio hilo, na hakuona vibaya kujisogeza katika ofisi za Clouds Fm asubuhi ya leo ili kukutana na kijana huyo na kuweza kumchangia chochote kidogo alichonacho.
Diamond Platnumz alitoa Tsh. Millioni 2 taslim na kumkabidhi kijana Said kama msaada wake kwa kijana huyo.
Sio Diamond Platnumz pekee ambae alihudhuria studioni hapo, bali pia Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Muheshimiwa Paul Makonda naye pia alihudhuria na kukabidhi Tsh Million 10 kama kutimiza ahadi yake aliyoahidi kumpa ndugu Said kama mtaji ambao utakuwa kama msingi katika kuendeleza maisha yake baada ya kupatwa na matatizo hayo.
Paul Makonda hakuishia kwenye millioni 10 tu, bali alitaja misaada mingine ambayo imetolewa na makampuni, taasisi pamoja na watu binafsi ambao amewatembelea kumuombea msaada kijana Said. Ambapo alitaja kuwa zimepatikana Pikipiki 5 ambazo zitafanya kazi kama Bodaboda kuhakikisha zinamuingizia kipato cha kila siku ndugu Saidi, Bajaji 2 pamoja na kuahidiwa kujengewa nyumba katika jiji la Dar es Salaam sehemu yoyote ile ambayo ndugu Said atahitaji.
Bado misaada inaendelea kupokelewa kwa yeyote aliyeguswa na hili na hii hapa ni namba ya account ambayo inapokea pesa za misaada ya ndugu Said-:
CRDB Bank Account 0152226886400 jina Said Ally
Tazama hapa chini jinsi ilivyokuwa studio humo baada ya Diamond Platnumz kuingia.
Jiunge na hatukwamii.blogspot.com/ sasa
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter naInstagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video
Mambo mengi yamezuka baada ya show ya Mombasa rocks festival ambayo mkali wa Marekani, Chris Brown alitumbuiza.
Moja likiwa ni suala la Alikiba kuzimiwa mic alipokuwa akitumbuiza huku akihoji uwepo wa meneja wa Diamond backstage.
Meneja wa Alikiba, Aidan na yeye ameamua kufafanua suala hilo lililoibua vita ya mashabiki wa mafahari hao wawili ambayo ilikuwa imeanza kupotea, “Sitaki kuingia sana kwenye ishu ya kuzimiwa MIC sijui nini, umeona! Ishu ni kwamba Ali, alianza na Nyimbo ya MacMuga, then AJE ni nyimbo ambayo kila siku huwa anaifungia shoo lakini alii-perfom akijua pale anatakiwa kumaliza kwa zile nyimbo mbili.” Aidan alifunguka kwenye kipindi cha Amplifaya . “Lakini yeye wakati anajiandaa kuwaambia watu kwamba he gonna be back on stage, MIC ikakatwa, ndio pale watu wakashindwa kuelewa kwanini Ali ameshuka! Lakini alikuwa anataka kuwaeleza kwamba atarudi, sababu muda ulikuwa haujitoshelezi.” . “Lakini hii ishu sio eti alizimiwa MIC sijui na Meneja wa Chris Brown, wenyewe walikuwa na time yao kabisa, wazungu wako proffesional.”
Alimaliza Aidan lakini pia aliligusia la Ali Kiba kuhoji uwepo wa Sallam SK, back stage. “Alichokizungumza Ali naomba kibaki kama alivyo kizungumza, I think kutokana na tension iliyopo baina ya wasanii wawili au kambi hizi mbili, I don’t think Kama kilikua kitu cha busara kwa Sallam au mtu anayetajwa kuwepo eneo lile kipindi haya mambo yanaendelea. Ingekua ni Mimi labda nimeenda kwenye shoo na msanii wangu hayupo, nisingekuwa NANG’AA NG’AA SANA PALE, Kutokana na kinaweza kutokea kitu chochote kibaya ukahusishwa.” . “Na ALI hajamtaja kuwa yeye ndio aliyefanya vile, watu wanajaribu kutoelewa! Ila ALI alikuwa anauliza WHY WAS HE DOING THERE? yani kibusara tu. Halikuwa jambo la busara kwa yule jamaa kuonekana pale.”
Jiunge na hatukwamii.blogspot.com/ sasa
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter naInstagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video
Wiki iliyopita msanii Diamond Platnumz alifanya interview na kipindi cha Jahazi cha Clouds fm.
Na moja kati ya mambo ambayo aliyazungumza mkali huyo ni pamoja na jinsi gani amejipanga kuondoa kero za upakuaji wa nyimbo katika mitandao.
Kitu ambacho alidai kuwa kinawakera wengi kutokana na kuwa na process ndefu kama kujisajili na vitu kama hivyo endapo mtu atahitaji kupakua wimbo na hivyo kumfanya mtu kupata shida wakati wa kupakua wimbo.
Diamond aliweka wazi mipango yake na team yake nzima kuwa wanajipanga kabla ya mwaka huu kuisha kuhakikisha wamewaletea mashabiki wao Platform ambayo itawawezesha kupata kazi zao kwa urahisi bila usumbufu kama ilivyo sasa.
“Kabla ya huu mwaka kuisha tutakuwa tuna App yetu sisi wenyewe na Platform au website ambayo zitapatikana nyimbo za Wasafi zote kiurahisi na bila kuwa na mlolongo mrefu. Tumeamu kufanya hivyo kwa kutambua kuwa watu wanatamani kupata nyimbo zetu lakini wanazipata kwa tabu sana. Na hivi sasa Platform hiyo iko inamaliziwa na pia tupo katika maongezi tu na baadhi ya makampuni kwasababu kuna baadhi ya kazi ambazo zitakuwa zinachajiwa kwa gharama ndogo tu kama Tsh. 50 au 100 tu mtu aweze kupata nyimbo.” Alisema Diamond Platnumz.
Jiunge na hatukwamii.blogspot.com/ sasa
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter naInstagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video
Baada ya habari kusambaa mtandaoni juu ya kifo cha mchekeshaji kutoka nchini Uganda, Kansiime Kubiryaba Anne maarufu kwa jina la Anne Kansiime, ambazo zilianzishwa na tovuti ya TimesLives.
Tovuti hiyo ilisema kuwa staa huyo alianguka jukwaani Jumapili hii akiwa Afrika Kusini na kukimbizwa hospital kabla umauti haujamfika ikiwa tu anaumri wa miaka 29.
Taarifa nikwamba Mchekeshaji Anne Kansiime ni mzima, kuthibitisha ilo ameamua kutumia ukurasa wake wa Facebook ambao upo verifaid kupinga tetesi hizo vikali ambapo aliweka wazi kwa mashabiki zake kuwa yupo hai na hajafa.
Pia aliwataka waandishi wa habari hiyo kufanya kazi iliyo sahihi kwa kumtafuta yeye mwenyewe na kama angekuwa kafa angeamka kuwajibu.
Anne Kansiime ameandika hivi kwenye ukurasa wake wa Facebook.. “ Hmmmmm….so times1ive.co.za please help me to help you! If you are going to tell my ninjas that am dead, atleast tell me in advance so I back up your story. Indeed Idleness has finally become a hobby. Well, relax my ninjas, your queen ninja is not about to desert you fwaaaaaa…..I still have alot of love and joy to give. #sharedblessings #IKnowWhoIam.”
Kwa wale ambao hawafahamu juu ya vichekesho vyake Anne Kansiime, hiki ni kimoja wapo.
Jiunge na hatukwamii.blogspot.com/ sasa
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter naInstagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video
Msanii wa Bongo fleva Diamond Platnumz ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake ‘Salome’ amefunguka na kusema kuwa wimbo huo uliwavuruga wasanii wengi wakubwa duniani kabla haujatoka hata baada ya kutoka.
Diamond Platnumz alisema hayo kwenye Friday Night Live (FNL) na kudai kuwa wimbo huo yeye mwenyewe anashindwa kuelewa una nini kutokana na jinsi ambavyo umeweza kupokelewa vizuri na kupendwa na watu wengi sana duniani.
“Kiukweli kabisa hata wakati napata wazo kusema nifanye wimbo wa ‘Salome’ nilikuwa nasema ni wimbo fulani mzuri kiasi kwamba hata mtu asipoelewa lugha lakini anaweza kuipenda, nakumbuka hata wakati Mama yule Saida Karoli alipoimba wimbo ule na ulipokuwa unavuma tulikuwa hatuelewi anazungumza nini lakini tuliipenda na ilikuwa nzuri na ilivuma sana, kwa hiyo nikasema kwa sasa hivi soko lilivyokuwa na nikiwatizama Watanzania nikichukua wimbo ule nikatia vitu vyangu fulani hivi itakuwa kali zaidi.
Saizi wimbo huu Afrika na sehemu ambazo wanatutizama imekuwa kubwa nafikiri watakuwa wameipenda sana hata ukiangalia ‘Comments’ zao kwenye video ile ‘Youtube’ unaona kuwa wameipenda.
Diamond aliendelea “Kabla ya wimbo kutoka Wizkid alikuwa Tanzania, wakati nipo naye nilimpa ule wimbo aisee ulimvuruga sana, nilipata bahati ya kumsikilizisha na Mh. Rais Mstaafu Jakaya Kikwete naye aliupenda sana, hata baada ya wimbo kutoka wasanii wakubwa kama wakina Teckno, Flavour walinitumia ujumbe mfupi kuonyesha kuupenda, nakumbuka hata Neyo naye aliniambia ‘I like the song ”.
Jiunge na hatukwamii.blogspot.com/ sasa
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter naInstagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video
Kiba amesema ni shabiki na mpenzi mkubwa wa mziki wa singeli lakini maneno na lugha wanazotumia katika nyimbo hizo zinamfanya asiufurahie mziki huo.
Kiba ameiambia Planetbongo kuwa mziki wa singeli kwa sasa unapendwa sana kwa hiyo ni wakati wa wasanii wake kutumia maneno yanayoweza kutumika katika maongezi ya kawaida.
Anasema licha ya kuupenda lakini huwa hasikilizi sana kwa kuhofia kumuathiri katika uandishi wake naye akajikuta anaandika maneno hayo ya wanasingeli ambayo ni lugha zisizokuwa na staha inayotakiwa.
AJE REMIX INAKUJA..
Kiba pia ameweka wazi kuwa video ya aje remix imeshakamilika ambayo wameifanya na rapa mnigeria M.I, lakini kiba amesema, ilibidi waongeze baadhi ya vionjo kwenye wimbo ili kuutofautisha na ule uliovuja.
Amedokeza video ina kucheza kwingi na anaonekana msichana mmoja tu na alikiba Kwenye video hiyo.
Aje ya AliKiba anayoitoa kama remix ndiyo ilikua toleo original lakini ikavuja kabla ya kutoka rasmi.
Jiunge na hatukwamii.blogspot.com/ sasa
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter naInstagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video
Mchekeshaji maarufu Duniani Kevin Hart anaungana na wasanii wengine wakubwa ambao majina yao yamepata heshima yakupata Nyota ya Hollywood Walk of Fame. Mchekeshaji huyo wa miaka 37 ambaye anajiaandaa kutengeneza filamu mpya ya Jumanji akiwa na The Rock, siku ya jumatatu ilikuwa ni furaha kwake baada ya jina lake kutajwa kupewa heshima ya nyota ya Hollywood Walk of Fame.
Wiki nyuma zilizopita Kevin Hart alitangazwa na mtandao wa Forbes kuwa ni moja ya wachekashaji ambao wanaingiza mtonyo mkubwa.
Jambo ambalo unapaswa kulifahamu ni kwamba kabla ya kuwa maarufu, Kevin Hart alikuwa akifanya kazi ya kuuza viatu, katika safari yake hiyo Kevin Hart aliamua kuiacha kazi hiyo na kuingia kwenye tasnia ya uchekeshaji akianzia kwenye matamasha ya stand up comedy katika kumbi za usiku.
Jiunge na hatukwamii.blogspot.com/ sasa
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter naInstagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video
Msanii wa Bongo Fleva Linah Sanga maarufu kama ‘Ndege Mnana’ amefunguka na kusema kwa sasa hana ujauzito kama ambavyo watu wanahisi ila amedai kuwa yeye mwenyewe anatamani kuwa na mtoto na kusema muda si mrefu huenda mambo yakawa hivyo.
Linah Sanga alisema hayo kupitia kipindi cha Friday Night Live ya EATV na kusema hivi sasa hana mimba ila soon mambo yanaweza kuwa hivyo kwani kwa sasa amejikita kufanya muziki na mambo ya msingi katika maisha yake.
“Hapana hii si mimba, nguo tu imesogea kwa mbele haya mambo huwa hayafichiki maana yataonekana tu, ila kiukweli soon mambo yanaweza kuwa hivyo. Maana saizi nimeamua kufanya muziki na mambo ya msingi, maana hata wazazi wetu wanafurahi kuona tukifanya mambo ya msingi kuliko mambo ya kijinga” alisema Linah Sanga.
Jiunge na hatukwamii.blogspot.com/ sasa
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter naInstagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video