Tuesday, October 11, 2016

KEVIN HART NDANI YA HOLLYWOOD WALK OF FAME



Mchekeshaji maarufu Duniani Kevin Hart anaungana na wasanii wengine wakubwa ambao majina yao yamepata heshima yakupata Nyota ya Hollywood Walk of Fame.
Mchekeshaji huyo wa miaka 37 ambaye anajiaandaa kutengeneza filamu mpya ya Jumanji akiwa na The Rock, siku ya jumatatu ilikuwa ni furaha kwake baada ya jina lake kutajwa kupewa heshima ya nyota ya Hollywood Walk of Fame.



Wiki nyuma zilizopita Kevin Hart alitangazwa na mtandao wa Forbes kuwa ni moja ya wachekashaji ambao wanaingiza mtonyo mkubwa.




Jambo ambalo unapaswa kulifahamu ni kwamba kabla ya kuwa maarufu, Kevin Hart alikuwa akifanya kazi ya kuuza viatu, katika safari yake hiyo Kevin Hart aliamua kuiacha kazi hiyo na kuingia kwenye tasnia ya uchekeshaji akianzia kwenye matamasha ya stand up comedy katika kumbi za usiku.



Jiunge na hatukwamii.blogspot.com/ sasa


Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video 

0 comments:

Post a Comment