Mwamuzi Anthony Taylor ameteuliwa kuchezesha mchezo wa mahasimu wa soka nchini Uingereza Liverpool dhidi ya Manchester United uliopangwa kuchezwa mwanzoni mwa juma lijalo.
Mwamuzi huyo mwenye umri wa miaka 37,
ameonekana kutokua na bahati na liverpool pale anapochezesha michezo inayoihusu klabu hiyo ya Anfield, kwani mara kadhaa anapopewa jukumu hilo majogoo wa jiji hufungwa ama kutoka sare.
ameonekana kutokua na bahati na liverpool pale anapochezesha michezo inayoihusu klabu hiyo ya Anfield, kwani mara kadhaa anapopewa jukumu hilo majogoo wa jiji hufungwa ama kutoka sare.
Mchezo unaokumbukwa ambao Liverpool walimaliza wakiwa washindi ulikua dhidi ya Stoke City waliokubali kufungwa bao moja kwa sifuri kwenye michuano ya kombe la ligi mwanzoni mwa mwaka huu, ambapo Teylor alikuwa msimamizi wa sheria 17.
Mchezo mwingine ambao ulishuhudia Liverpool wakichomoza na ushindi huku Taylor akipuluza kipyenga ulikua dhidi ya Swansea city uliochezwa mwezi Novemba mwaka 2015.
Hata hivyo kwa upande wa Man Utd, mambo
huonekana kuwa tofauti pale muamuzi huyo
anapochezesha michezo yao ambapo mara zote wamekua wakiibuka na ushindi na inapotokea matokeo ya sare basi huchukuliwa kama bahati mbaya.
huonekana kuwa tofauti pale muamuzi huyo
anapochezesha michezo yao ambapo mara zote wamekua wakiibuka na ushindi na inapotokea matokeo ya sare basi huchukuliwa kama bahati mbaya.
Lakini pamoja na tathmini hiyo kutolewa bado Taylor anaendelea kutajwa kama mwamuzi ambaye hana mapenzi na klabu yoyote inayoshiriki ligi kuu ya soka nchini Uingereza, licha ya makazi yake kuwa na umbali wa maili sita kutoka uwanja wa Old Trafford.
Kwa msimu huu, mwamuzi huyo tayari
ameshachezesha michezo saba na ametoa kadi 23 za manjano.
ameshachezesha michezo saba na ametoa kadi 23 za manjano.
Wakati chama cha soka nchini Uingereza
wakifanya maamuzi ya kumteua Taylor
kuchezesha mchezo huo, bado wanaendelea
kukumbukwa kwa hatua waliyoichukua ya
kubadilisha jina la mwamuzi huyo siku chache kabla ya mchezo wa nusu fainali ya kombe la FA kati ya Man Utd dhidi ya Everton msimu uliopita, kufuatia malalamiko ambayo yalitolewa na mashabiki ya kuonyesha hawana imani naye.

Suala la malalamiko ya mashabiki tayari limeanza kuchukua nafasi kubwa kuelekea mchezo wa mwanzoni mwa juma lijalo, kupitia mitandao ya kijamii na wengi walioonyesha kuchukizwa na uteuzi wa mwamuzi huyo ni manazi wa Liverpool.
Jiunge na hatukwamii.blogspot.com/ sasa
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video
0 comments:
Post a Comment