Thursday, September 29, 2016

YEMI ALADE AENDA KUSHOOT VIDEO MPYA ‘LOCATION’ ILEILE ALIYOITUMIA MICHAEL JACKSON


Staa wa Nigeria, Yemi Alade ameenda brazil kushoot video mpya kwenye location ileile aliyoitumia Michael Jackson miaka 20 iliyopita.

Yemi Alade anshoot video hiyo eneo la ‘favela of Dona Marta’ eneo ambalo King of Pop, marehemu Michael Jackson alishoot video yake ya utata ya ‘They Dont care about us’, wakati anashoot video hiyo serikali ya Brazil ilitaka kumzuia kwasababu kipindi icho mji wa Rio haukuwa mkubwa na waliamini hataitangaza nchi yao vizuri.

Yemi Alade yupo nchini humo kushoot video mpya ya wimbo unaoitwa ‘Make The Tuture’ pamoja na mastaa wengine watano ikiwemo Jennifer Hudson, Pixie Lott, Steve Aoki, Tan Wei Wei na Luan Santana.

0 comments:

Post a Comment