Thursday, October 6, 2016

Talaka haituzuii kufanya kazi pamoja tena..Jennifer Lopez &Marc Anthony


Ni miaka mitano sasa tangu kuvunjika kwa ndoa ya mrembo mwanamziki na muigizaji Jennifer Lopez na Mark Anthony iliyodumu kwa miaka saba. Kampuni ya mziki ya Marc Anthony Magnus Media pamoja na Sony Music Latin imetangaza kusaini mkataba wa biashara na Jlo.
Kampuni hizo mbili zitahusika kwenye usimamizi wa albamu ya Jlo ambayo ataimba kwa lugha ya Kihispania na ana mpango wa kuitoa november 2016.
Jlo anasema ana furaha na hamu ya kuanza safari hii ya mziki na kampuni hizo mbili, huku Marc Anthony akimuunga mkono kwa kusema Jlo amekuwa mwanamke mchapakazi na anayewakilisha utamaduni wa nchi yao duniani hivyo ni heshima kubwa kwake kuendeleza hili na atafanya naye kazi kwa ushirikiano na ubunifu ili kuendeleza historia nzuri.

Jlo na Marc Anthony kwenye harusi yao waliyoifanya kwa siri 2004 Beverly Hills
Kama ulikuwa hufahamu, Jennifer Lopez na Marc Anthony waliwahi kuwa marafiki wa karibu miaka ya 90 baadae mwaka 2004 wakatangaza uhusiano wao wazi kipindi ambacho Jlo akikatisha uchumba na aliyekuwa mpenzi wake, Ben Affleck huku Marc akiwa amepeana talaka na aliyekuwa mkewe Dayanara Torres.

Jiunge na hatukwamii.blogspot.com/ sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video 

0 comments:

Post a Comment