Pasi na shaka Ndege aina ya Bombardier Q400 zenye uwezo wa kubeba abiria 76 zilizotengenezwa nchini Canada ndio mkombozi sahihi kwa Watanzania kwani kwa kipindi kirefu sasa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) lilishindwa kujiendesha kutokana na sababu kadha wa kadha ikiwemo gharama za uendeshaji.
Moja ya sifa kuu ya ndege hii ni kuwa na uwezo wa kutumia mafuta kidogo, jambo litakalosaidia kupunguza gharama za usafiri huo wa ndege nchini kwa wasafiri wa ndani pamoja na kurahisisha mazingira ya uendeshaji; hadi sasa tayari zimekwisha wasili ndege mbili ambapo kesho zitazinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi) Dk. Leornard Chamuriho amesema maandalizi yote kwa ajili ya uzinduzi wa ndege hizo yamekamilika na uzinduzi huo utafanyika kesho kuanzia saa mbili asubuhi.
“Tunawaomba wanahabari na wananchi kujitokeza kwa wingi katika uzinduzi huo ili waone utekelezaji wa ahadi za serikali katika mkakati wa kuhuisha usafiri wa anga hapa nchini”, amesema Dk. Chamuriho.
0 comments:
Post a Comment