Ikiwa ni Octoba Mosi siku ambayo, imeshuhudiwa maeneo mbalimbali ya Jijini Dar es Salaam na Wilaya zake tano za Temeke, Ilala, Kinondoni, Ubungo na Kigamboni yakitekeleza agizo la Mkuu wa Mkoa huo Paul Makonda katika suala zima la upandaji wa Miti kupitia kampeni yake ya Mtiwangu.
Kampeni hiyo ambayo imezinduliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu, imeambatana na jambo lingine ambalo litawanufaisha wakazi wa Ilala na watanzania kwa ujumla.
Akizungumza juu ya suala hilo Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema ameelza kuwa kwa kushirikiana na kampuni ya mtandao wa simu ya TTCL wameweza kuweka ‘Internet’ ya bure kwa wakazi watakao kuwa wanaotembelea maeneo yenye bustani kubwa za mji, jambo litakalo wasaidia kupata taarifa mbalimbali zenye kuelimisha na kuwasiliana kupitia mitandao ya kijamii, ambapo Mkurugenzi wa TTCL Waziri Kindamba ameasema zoezi hilo halitakuwa la kusuasua kwani wamejipanga kufanya mapinduzi ya kimtandao na kuongeza kuwa Tanzania inakuwa nchi ya Tatu Afrika Mashariki kwa kufanya hivyo ikiungana na Kenya, Uganda, huku kwa Afrika ikiwa ya Tano zikiongezeka Nigeria na Afrika Kusini.
Kwa upande wake Makamu wa Rais amepongeza uwepo huo wa ‘Internet’ (WiFi) kwa maeneo yenye bustani ikiwemo NBC, Palm Beach, Mnazi Mmoja na Gymkana ambapo uzinduzi huo ulifanyika, huku akisisitiza suala la kutunza mazingira na upandaji miti liwe endelevu, kwani hali ya hewa ya Dar es Salaam imekuwa ya joto kutokana na athari za Mazingira, hivyo ameziagiza Wizara zinazosimamia Misitu na Mazingira kuzifuatilia bustani zote zilizopandwa miti siku ya leo.
0 comments:
Post a Comment