Tuesday, October 4, 2016

URUSI YASITISHA MKATABA WA NYUKLIA BAINA YAKE NA MAREKANI


Mkataba baina ya Urusi na Marekani ambao unahusisha silaha za kinyuklia umesitishwa rasmi na nchi ya Urusi huku hali hiyo ikipelekea kuzorota kwa uhusiano baina ya nchi hizo mbili.

Urusi kupitia kwa Rais wake Vladimir Putin imesema imeamua kuchukua hatua hiyo ili kulinda usalama wa Urusi huku akiituhumu Marekani kwa kuunda vikwazo vyenye kutishia uthabiti kwa kuchukua hatua zisizo za kirafiki dhidi ya nchi yake.




Urusi pia imetoa masharti ambayo lazima yafuatwe na Marekani kabla ya kurejelewa kwa mkataba huo ambapo mwaka 2000 walikubaliana kila taifa kuangamiza tani 34 za madini ya Plutonium ambayo hutumika kutengeneza silaha za kinyuklia ambapo huo ulikuwa mpango wakimataifa wa kupunguza silaha za nyuklia duniani

Masharti iliyotoa Urusi kwa Marekani ni pamoja na kuitaka nchi hiyo kuondoa vikwazo vyote vilivyowekwa na nchi hiyo dhidi ya Urusi na kulipwa fidia iliyotokana na madhara yaliyojitokeza baada ya vikwazo hivyo. Pia imetaka Kupunguzwa kwa wanajeshi wa Marekani na silaha zake katika nchi zilizojiunga na Nato baada ya 1 Septemba 2000

Itakumbukwa Marekani pamoja na nchi za umoja wa ulaya waliiwekea Urusi vikwazo kufuatia hatua ya nchi hiyo kuchukua jimbo la Crimea kutoka kwa Ukraine mwaka 2014 pamoja na hatua ya nchi hiyo ya kuunga mkono wapiganaji wanaotaka kujitenga kwa maeneo ya mashariki mwa nchi ya Ukraine


0 comments:

Post a Comment