Taarifa hii imetokea mianzini Arusha ambapo ndani ya nyumba aliyokuwa anaishi Christopher Akoonay baada ya kubomolewa wakati wa zoezi la upanuzi wa barabara na kikubwa kilichojitokeza ni mifuko ya plastiki iliyosheheni mamilioni ya fedha ambayo ilikuwa imechimbiwa chini ya ardhi .
Imeelezwa kuwa wapita njia na wakazi wa eneo hilo walipata neema ya kuokota fedha baada ya trekta lililokuwa likichimba barabara kuzichimbuwa na zikawa zimesambaa, lakini pia kuligeuka kilio kwa mmiliki wa hazina hiyo Christopher Akoonay.
Siku ya tukio, Akoonaay alikuwa yuko kwenye shuguli zake za kuwapelekea maziwa wateja wake ndipo watengeneza barabara walipofika kutengeneza barabara na kuanza kuichimba njia hiyo.
Christopher Akoonay ambaye amekuwa akizitunza pesa hizo chini ya ardhi tangu mwaka 2014 amesema alikuwa akiweka shilingi laki saba kila mwezi.
Gazeti la Habari Leo limeripoti kuwa nyumba ya Akoonaay ni miongoni mwa zile zilizobomolewa na ni baada ya wamiliki wake, kugoma kuzibomoa wenyewe ili kupisha upanuzi wa barabara hiyo.
0 comments:
Post a Comment