Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amezitaka taasisi na mashirika ya umma jijini hapa kuiunga mkono Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) kwa kutumia mawasiliano yanayotolewa na kampuni hiyo.
Kauli hiyo imetolewa Dar es Salaam alipokuwa akizindua wiki ya huduma kwa wateja wa TTCL.
“Serikali imeonyesha nia njema ya kuirejesha TTCL katika hali nzuri baada ya kuimiliki kwa asilimia 100. Kwahiyo litakuwa jambo la busara na la heshima kama mashirika na taasisi za umma zilizoko Dar es Salaam zitaunga mkono juhudi za Rais, Dk. John Magufuli za kuirejesha kampuni hiyo chini ya umiliki wa serikali kwa asilimia 100,” alisema Makonda.
“Katika hili, mimi kama kiongozi wa mkoa nitahakikisha ofisi zote za umma zilizopo chini yangu zinatumia huduma za TTCL kuimarisha uzalendo,” alisisitiza.
Aidha Makonda alizitaka taasisi za umma zinazodaiwa na kampuni hiyo zilipe madeni yao ili kampuni hiyo iweze kujiendesha kwa mafanikio.
BY:EMMY MWAIPOPO
0 comments:
Post a Comment