Kamati ya katiba, Sheria na hadhi za wachezaji ya shirikisho la soka Tanzania (TFF) ilimaliza kikao chake na klabu ya Simba usiku wa kuamkia leo na Simba inaendelea kubaki na pointi ilizopewa na Kagera Sugar.
Katibu Mkuu wa TFF, Selestine Mwesigwa (kulia) akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya kuahirisha kikao.
Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Celestine, amesema kamati hiyo itakaa tena na kuna shahidi wengine wataitwa kuhojiwa. “Kuna watu wanatakiwa kuhojiwa, kamati itakaa wiki hii. Tunawatafuta wahusika na wakipatikana itapangwa siku. Baada ya hapo kamati itatoa maamuzi,” alisema Mwesigwa.
Kikao hicho kilifanyika kuanzia asubuhi katika hoteli ya Protea jijini Dar es Salaam na waamuzi, wafanyakazi wa bodi ya ligi, viongozi wa simba, Kagera Sugar, waamuzi wa mechi kati ya Kagera Sugar dhidi ya African Lyon na beki Mohammed Fakhi wamehojiwa.
Baada ya kuhojiwa, kilichofuatia lilikuwa ni suala la kamati kukaa kwa takribani saa moja kuonyesha walikuwa wakimalizia kuhusiana na kile walichowahoji wahusika.
Kabla, kamati ya Saa 72, ilikuwa imeipa Simba pointi tatu na mabao matatu licha ya kufungwa kwa mabao 2-1 dhidi ya Kagera Sugar.
Kamati ya Saa 72, ilibaini Kagera Sugar ilimchezesha Fakhi mechi hiyo kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba akiwa na kadi tatu za njano.
Lakini Kagera Sugar wakaendelea kusisitiza kwamba Fakhi alikuwa na kadi mbili tu za njano alizopewa katika mechi ya Mbeya City na ile dhidi ya Majimaji na si dhidi ya African Lyon.
Na mchezaji Venance Ludovic ameidhinishwa kuwa mchezaji halali wa African Lyon.
Katiba, Sheria na hadhi za wachezaji ya shirikisho la soka Tanzania (TFF) imepitisha uamuzi huo katika kikao kilichofanyika jijini Dar es Salaam.
Lakini Lyon wamepigwa faini ya Sh 500,000 kutokana na kuonekana kuwa hawakufuata utaratibu katika usajili wake.
Mchezaji huyo alikuwa akilalamikiwa kwamba hakukamilisha usajili wakati anajiunga Lyon akitokea Mbao FC.
Lakini yeye alilalamika kwamba Mbao FC walivunja mkataba kwa kushindwa kumyima stahiki zake.
Tuandikie Maoni Yako Hapa Chini. Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video za kufurahisha na kuvunja mbavu.
0 comments:
Post a Comment