Rais Mstaafu wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete bado anaendelea kulitumikia bara la Afrika ambapo kama haufahamu, yeye pia ni Mjumbe maalum wa umoja wa Afrika katika usuluhishi wa mgogoro wa Libya.
JK ameshiriki mkutano wa kamati ya wakuu wa nchi wa umoja wa Afrika kuhusu Libya iliyokutana Brazaville, Congo chini ya uenyekiti wa Rais wa Congo Brazaville Dennis Sassou Ngueso ambapo kamati hiyo inaundwa na Marais wa Congo Brazaville, Afrika Kusini, Chad na Mauritania.
Mkutano huo uliitishwa kwa lengo la kupokea taarifa ya usuluhishi wa mgogoro huo na kuweka msimamo wa umoja wa Afrika katika utafutaji wa suluhu katika mgogoro wa Libya.
Kamati hiyo itawasilisha taarifa yake katika mkutano wa wakuu wa nchi wa baraza la usalama la Umoja wa Afrika Addis Ababa pembezoni mwa mkutano wa wakuu wa nchi za umoja wa Afrika unaotarajiwa kufanyika Addis Ababa tarehe 30 na 31 January 2017.

Caption 1: Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete katika Mkutano wa Kamati ya Wakuu wa Nchi za AU kuhusu Libya. Kulia kwake ni Rais wa Mauritania na Mwenyekiti na Rais wa Congo, Mhe. Dennis Sassou Ngueso.
Caption 2: Rais Mstaafu Dkt Jakaya Kikwete akisalimiana na Rais wa Chad na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika na Rais Mhe. Idriss Deby.
0 comments:
Post a Comment