Thursday, April 6, 2017

Juventus yaingia fainali ya Copa Italia

klabu ya Turin Juventus imefanikiwa kutinga katika hatua ya fainali ya kombe la Copa italia licha ya kufungwa na Napoli kwa 3-2 katika mchezo wa nusu fainali ya pili.
Juventus wamesonga mbele kwa jumla ya mabao 5-4, baada ya nusu fainali ya kwanza kushinda kwa mabao 3-1.
Mchezo wa fainali utawakutanisha Juventus na Lazio na mchezo huo utapigwa june 2 mwaka huu. Katika uwanja wa Olimpico.
Mshambuliajia wa Juventus ambaye ni raia wa Argentina Gonzalo Higuain ndie aliyefunga mabao yote mawili kwa timu yake huku mabao ya Napoli yakifungwa na mshambuliaji Marek Hamsik na Dries Mertens akifunga bao la pili huku Lorenzo Insigneakifunga bao la tatu.

Source:bongo5
Tuandikie Maoni Yako Hapa Chini. Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video za kufurahisha na kuvunja mbavu.

0 comments:

Post a Comment