Thursday, April 6, 2017

Walichokiandika Nay wa Mitego na Zitto baada ya Roma kukamatwa


Baada ya Mbunge wa Mikumi na staa Bongo Fleva Joseph Haule ‘Prof Jay’ kutoa taarifa kupitia account yake ya Instagram kuhusu kukamatwa kwa staa mwingine wa Hip Hop Roma Mkatoliki katika studio za Tongwe Records na watu wasiojulikana, taarifa hiyo imeamsha hisia za watu mbalimbali wakiwepo mastaa wa Bongo Fleva na wanasiasa.
Leo April 6 2017 kupitia account zao za Instgram na Twitter Rapa Nay wa Mitego na Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe wameyaandika haya..>>>”Kuvamia Ofisi Za watu, heh.! Kumbe nayo ni Kazi.?! Nina Imani uko salama mwanangu, Kamanda @roma2030 Sina ata chembe ya wasi wasi. #Wapo.” – Nay wa Mitego.
>>>”Uvamizi wa studio ya Tongwe na kumkamata msanii Roma Mkatoliki ni mwendelezo wa uongozi wa kigangstar na lazima kulaani Kwa nguvu zetu zote.” – Zitto Kabwe.
Source:millardayo
Tuandikie Maoni Yako Hapa Chini. Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video za kufurahisha na kuvunja mbavu.

0 comments:

Post a Comment