Kuna usemi mmoja wa Kiswahili unasema, ‘vita vya panzi furaha kwa kunguru’, usemi huu unakwenda sambamba na hali iliyojitokeza kwenye baadhi ya vituo vya kuuzia tiketi za mfumo mpya wa tiketi za ki-electronic ‘electronic ticketing’ ambapo ilifika wakati kadi za Selcom zikaanza kuunzwa.
Kwenye baadhi ya vituo, kadi hizo zilipungua ukilinganisha na mahitaji ya wateja ambao walikuwa wakisubiri kupewa kadi hizo ili wakate tiketi kwa ajili ya kushuhudia pambano la Yanga na Simba ambapo zimebaki saa kadhaa tu ili timu hizo zioneshane kazi.
Wadau ambao walikuwa wakisubiri kuhudumiwa kwa utaratibu huo wamethibitisha baadhi ya mawaklala wa Selcom kuziuza kadi hizo pale ilipotokea mahitaji yalikuwa ni makubwa huku kadi zikiwa chache.
“Utaratibu wa kugawa kadi ulikuwa si mzuri kwasababu asubuhi (jana) tumekuja tukijua tutapewa kadi bure lakini tukawa tunauziwa kadi kwa shilindi 3000 badala ya bure, baada ya watu kulalamika zikaja gari mbili aina ya Noah wakaingia ndani, unaenda unatoa shilingi 7000 unapewa kadi bure na tiketi, matatizo sasahivi yameisha”, anasema Hamad Salum mmoja wa mashabiki aliyekumbana na adha ya kupata tiketi.
“Kwa asubuhi utaratibu ulitusumbua sana kwasababu nilikuja hapa mida ya saa 2 (jana) hali ilkuwa ngumu hakuna kadi wala tiketi, ilifika kipindi tulikuwa tunanua kadi shilingi 3000 lakini baada ya watu kulalamika na vurugu kutokea, wakaleta magari sasahivi utaratibu unaendelea izuri”, Ramadhani Singilimo mdau mwingine aliyeuziwa kadi ya selcom.
“Nipo hapa tangu saa 2 asubuhi (jana) nakata tiketi, tatizo foleni na kadi hazipatikani kwa wepesi, hadi utoe hela, tiketi ya 7000 unatoa 10000 ndio unapata tiketi. Inabidi utoe hela nyingi watu wakufanyie mipango upate tiketi. Umeshakuwa wizi tayari, unatoa shilingi 10000 unapata tiketi ya 7000”, Azam Ligola.
Awali Selcom walitangaza kutoa kadi hizo bure huku mteja akitakiwa kukunua tiketi pekee ili kuangalia mtanange wa Yanga na Simba ikiwa ndiyo mchezo pekee wa kwanza wa ligi msimu huu kushuhudiwa huku watazamaji wakitakiwa kutumia mfumo mpya wa tiketi za electronic.
0 comments:
Post a Comment