Friday, September 30, 2016

Dully Sykes: ‘Inde’ haijanipa mafanikio yoyote kwa sasa

Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva, Dully Sykes amesema kuwa hakuna mafanikio aliyoyapata kwa sasa kupitia wimbo wake mpya wa ‘Inde’.


Muimbaji huyo ni mmoja kati wa wasanii wa muda mrefu kwenye tasnia ya muziki ikiwa ni zaidi ya miaka 15 lakini mpaka leo hii anaendelea kufanya vizuri kwa kuachia hit kibao.
Akiongea na mtangazaji wa redio Maisha ya Dodoma, Silver Touchez kwenye kipindi cha Flavour Express, muimbaji huyo amesema, “‘Inde’ haijanipa mafanikio yoyote mpaka sasa kwakuwa ndio naanza kufanya show. Baada ya miezi sita nitakuwa na jibu zuri juu ya mafanikio ya wimbo huo.”
Mpaka sasa wimbo huo umeshatazamwa kwa zaidi ya milioni 1.9 kwenye mtandao wa Youtube tangu utoke mwezi Agosti, mwaka huu.

0 comments:

Post a Comment