Ligi Kuu England msimu wa 2016/2017 iliendelea usiku wa April 5 2017 kwa michezo sita kuchezwa, mchezo kati ya Arsenal dhidi ya West Ham United ni miongoni mwa michezo iliyochezwa usiku wa April 5, licha ya watu wengi kufuatilia game ya Man City vs Chelsea lakini game ya Arsenal ilikuwa na mvuto wake pia.
Wengi walikuwa wakifuatilia game ya Chelsea dhidi ya Man City iliyochezwa katika uwanja wa Stamford Bridge na kumalizika kwa Chelsea kupata ushindi wa goli 2-1, Arsenal usiku huo pia walifanikiwa kupata ushindi wao wa kwanza wa EPL baada ya siku 53 bila ushindi.
Arsenal wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani wa Emirates wamefanikiwa kupata ushindi wa goli 3-0 dhidi ya West Ham United ushindi ambao umeiwezesha kurudi nafasi ya tano na kuishusha Man United hadi nafasi ya 6.
Matokeo ya mechi za #EPL zilizochezwa usiku wa April 5 2017 #MillardAyoUPDATES
Magoli ya Arsenal yalifungwa dakika ya 58 na Mesut Ozil, Theo Walcott alifunga goli la pili dakika ya 68 kabla ya Oliver Giroud kufunga goli la tatu lililoirudisha Arsenal katika nafasi ya 5.
Msimamo wa #EPL baada ya kuchezwa mechi za April 5 2017 #MillardAyoUPDATES
Source:millardayo
Tuandikie Maoni Yako Hapa Chini. Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video za kufurahisha na kuvunja mbavu.
0 comments:
Post a Comment