Wednesday, April 19, 2017

Daladala Yagonga Treni Leo Alfajiri Dar es Salaam na Kusababisha Maafa

Mtu mmoja amefariki dunia baada ya kutokea ajali ya basi la abiria/daladala (T 435 DGG) kutoka Gongo la Mboto kwenda Mnazi Mmoja kuigonga treni ya Pugu leo Aprili 19, 2017 saa 11 alfajiri katika makutano ya reli na barabara ya Nkurumah jijini Dar es Salaam.

Majeruhi wa ajali ni 23 , wanane wapo hospitali ya Amana na waliobakia 15 wapo Hospitali ya Taifa Muhimbili MOI watatu kati yao ni mahututi. Taarifa zaidi itatolewa kuhusu ajali hiyo.

Hata hivyo treni ya Pugu inaendelea na huduma zake kwa kufuata ratiba.

Imetolewa na Afisi ya Uhusiano kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TRL

Nd. Focus Sahani,
Dar es Salaam,
Aprili 19, 2017.



Tuandikie Maoni Yako Hapa Chini. Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video za kufurahisha na kuvunja mbavu.

0 comments:

Post a Comment