Thursday, April 20, 2017

Shabiki wa Yanga amemtolea uvivu Haji Manara, amejibu mapigo yake

Kwanza Manara unanishangaza mpaka nafikia kukudharau kwa namna unavyotumia nguvu nyingi kuaminisha watu wa soka kwamba unatimu nzuri kiasi hakuna mfanowe hapa Tanzania rejea kauli ya “This is Simba”.
Manara nakuhakikishia una team mbovu kuliko unavyofikiria, kitu pekee mlichoweza kufanikiwa ni kuunganisha mashabiki wenu waliokuwa wamepotea kwa kukosa ubingwa kwa miaka kandhaa. Morali ni muhimu sana kwa club yoyote ndio maana hufikia hatua Shabiki kuitwa ni mchezaji wa 12, hilo umefanikiwa kiasi cha kila unachokiongea wanachama wako hudhani kinaukweli kumbe ni uongo na kujitafutia pakujificha.
Ushahidi wa hili nisemalo ni mechi zenu mlizocheza anzia Mbeya City, Dodoma Mbuzi Mup, Madini FC, Kagera Sugar, Mbao FC na Toto African. Hizi mechi ndizo zinatafsiri ubora na ubovu wa Simba, Kagera kakupiga kweupeeeee ‘mipovu’ tu yakutoka. Acha kuropoka manara wewe ni mtu mzima sasa.
Hoja yako ya pili ni suala la Mkemi kuitishia TFF…wewe jamaa uwe na kumbukumbu, ulishatoa kauli chafu sana zinazoishutumu TFF moja kwa moja tena bila weledi katika soka.
Zikumbuke hizi; “Liwe jua, iwe mvua tutapambana na Yanga na fitina za TFF mpak atubebe kombe.” “Tunawaambia TFF waache kuibeba Yanga na kuanzia sasa mechi zote na Yanga tunataka refa atoke nje ya TANZANIA.” (shinikizo la kitoto kabisa maana hata kanuni za mashindano husomi).
Kauli ya Mkemi ipo ‘very open’ mpaka sasa kuna harufu ya rushwa, haiwezekani kadi poorer ipotee, haiwezekani kadi isionekane kwa baadhi na baadhi ionekane na ‘it seems’ mamlaka za TAKUKURU, na hata Polisi wenye dhamana ya uchunguzi au udukuzi wowote wa simu au ‘cyber crimes’ waingilie kati juu ya suala hili maana kamati zote zinashindwa…Manara acha kuropoka Mkemi was well and clear.
Hoja yako ya tatu ni upendeleo unaodai Yanga wanapewa na TFF, hivi manara katika hali ya kawaida uondoe ushabiki japo kwa sekunde tu uone upendeleo ulioupata wewe wa kupewa mechi 7 at the same ground, tena kiwanja cha nyumbani, ulikaa kimya huku ukichekelea na kutamba na hiyo kitu ona unavyoumbuka game za away!
Ulipiga sana kelele za refa wa Yanga na Simba, afungiiwe kisa kumpa kadi nyekundu Mkude ‘but you didn’t mention’ ngumi ya Banda kwa Makapu, kumbe hata wew hujui kutenda haki?
Ulipiga sana kelele kwa refa wa Majimaji vs Yanga afungiwe ambaye hakuona tukio la Abdul kuunawa mpira katika box ‘but you didn’t mention’ ngumi ya Banda kwa Kavila ili yule refa afungiwe nae maana nae naskia hakuona.
Manara acha kuropoka kama kupendelewa wewe pia unapendelewa…
Hoja ya wwe ni mtoto wa mjini na utamwaga ugali, hilo ni kujidhalilisha mbele za familia ya soka, ikiwa kuna lolote ulilijua kuwa Yanga walilifanya na ukalikalia kimya basi ujinga ni wako, maana wewe ilitakiwa kupeleka mashitaka yako unapoona utapata haki yako na sio kufanya press conference ili kuwajuza watu kuwa utapiga teke sahani.
Halafu kingine Manara cha mwisho, wewe una exposure kubwa ya ethics za soka, una-access kubwa ya namna ya kusimamia soka duniani kote lakini mbona ukiwa ‘front of the mic’ unaongea vitu ambavyo huendani navyo unaongea point ‘cheap’ sana, unaita watu ‘gongowazi’ na utani wa ajabu sana mpaka juzi nimeona alichokijibu Wema Sepetu.
Hivi watu wakiamua na wewe kukutania kweli utahimili UTANI wewe!!?
Hebu ongea ‘FACTS’
source:shaffihdauda
Tuandikie Maoni Yako Hapa Chini. Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video za kufurahisha na kuvunja mbavu.

0 comments:

Post a Comment