Friday, April 14, 2017

Waliovunjiwa nyumba Mkwajuni Dar kulipwa

BUNGE limeelezwa kuwa wananchi waliovunjiwa nyumba katika eneo la Mkwajuni wilayani Kinondoni ambao wana hati watalipwa fidia.

Kauli hiyo ilitolewa na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula, wakati akijibu swali la Mbunge wa Kinondoni, Maulid Mtulia (CUF) aliyetaka kujua hatima ya watu waliovunjiwa nyumba katika eneo hilo.
Naibu Waziri alisema, ni kweli watu walivunjiwa nyumba katika eneo la Mkwajuni na Mkunguni, hivyo wapeleke hati zao wizarani walipwe fidia.
Akijibu swali la msingi la Mbunge wa Viti Maalumu, Salma Mwassa (CUF) aliyetaka kujua kuna umuhimu gani kusarisimisha nyumba alisema, kunapunguza migogoro ya ardhi.
Mabula alisema urasimishaji wa ardhi maana yake ni kutambua miliki ya wananchi kwenye maeneo yaliyoendelezwa bila kupimwa kisheria.
Matokeo ya urasimishaji ni kutoa hati miliki na kuweka miundombinu ya msingi kama vile barabara, maji, mifereji ya maji ya mvua na ikiwezekana majina ya mitaa.
“Urasimashaji ni mpango shirikishi unaowezesha wananchi kukubaliana na mipaka ya viwanja, kufungua njia na kutoa maeneo ya huduma za jamii kama vile shule, vituo vidogo vya polis, makaburi, zahanati na maeneo ya wazi,” alisema.

source:habarileo
Tuandikie Maoni Yako Hapa Chini. Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video za kufurahisha na kuvunja mbavu.

0 comments:

Post a Comment