Nahodha wa timu ya taifa ya Brazil anayeichezea klabu ya FC Barcelona ya HispaniaNeymar jina lake limeingia kwenye headlines baada ya mtandao wa Besoccer kuripoti stori tofauti na ilivyokuwa imeripotiwa na baadhi ya mitandao siku kadhaa nyuma.
Awali Neymar aliripotiwa kuongeza mkataba na FC Barcelona hadi 2021 licha ya kuwa sio yeye wala viongozi wa FC Barcelona ambao waliongea na waandishi wa habari kuhusiana na suala hilo tofauti na ilivyozoeleka.
Neymar yuko radhi kuongeza mkataba wa kuitumikia FC Barcelona hadi 2021 wenye thamani ya euro milioni 250 ambao utamfanya alipwe mshahara wa euro milioni 15 kwa mwaka, dili la Neymar na FC Barcelona lilikuwa likamilike toka July 15 2016 lakini bado haijawekwa wazi nini kilikwamisha.
0 comments:
Post a Comment