Wednesday, October 5, 2016

RAIS DKT MAGUFULI AMWANDALIA DHIFA YA TAIFA RAIS JOSEPH KABILA WA DRC, IKULU


 Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Joseph Kabila akigonganisha glasi kumtakia heri mwenyeji wake Rais Dkt Magufuli wakati wa dhifa ya Taifa iliyoandaliwa kwa heshima yake Ikulu jijini Dar es salaam


Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Joseph Kabila akigonganisha glasi na Mama Janeth Magufuli kumtakia heri yeye na mwenyeji wake Rais Dkt Magufuli wakati wa dhifa ya Taifa iliyoandaliwa kwa heshima yake Ikulu jijini Dar es salaam


Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Joseph Kabila akigonganisha glasi na makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na mwenyeji wake Rais Dkt Magufuli wakati wa dhifa ya Taifa iliyoandaliwa kwa heshima yake Ikulu jijini Dar es salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Joseph Kabila wakitumbuizwa na kikundi cha Brass band cha Mount Usambara chini ya Mzee Hoza Ikulu jijini Dar es salaam


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akionesha umahiri wake wa kupiga ngoma mbele ya Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho kikwete baada ya dhifa hiyo ya Kitaifa.

0 comments:

Post a Comment