Mkali wa wimbo ‘Salome’ na Mkurugenzi wa WCB, Diamond Platnumz amesema uwekezaji mkubwa alioufanya katika label yake ya ‘WCB’ hauwezi kumlipa kwa muda mfupi.
Label hiyo ambayo kwa sasa inafanya vizuri katika muziki ina wasanii 4, Rich Mavoko, Harmonize, Rayvanny pamoja na Queen Darlin.
Akiongea katika kipindi cha The Playlist cha Times FM, Diamond alisema label hiyo kwa sasa inatumia pesa nyingi kuliko kuingiza.
“Bado sana haiwezi kulipa kwa muda mfupi, itachukua mwaka mmoja mpaka miwili ndo inanze kulipa lakini sasa hivi bado,” alisema. “Lakini furaha yangu ni kuona wasanii wa WCB wanaanza kuwa nominated kwenye tuzo tofauti tofauti za Afrika, nyimbo zao zinatambulika katika nchi tofauti za Afrika, wanatambulika na wasanii tofauti tofauti wa Afrika, so hicho ndio kitu ambacho nilikuwa nakipigania,”
Pia muimbaji alisema ameamua kusaidia wasanii kwanza alafu swala la mapato litakuja baadae wakati wasanii wapo kwenye ramani ya muziki.
0 comments:
Post a Comment