Monday, November 28, 2016

Unajua jezi ya Madrid ya jana imetengenezwa na nini? sababu ya kuvaa jezi hizo je? Ingia hapa

Wanasema ilikuwa business as usual jana katika Uwanja wa Santiago Bernabeu, wakati Cristiano Ronaldo alitumbukiza mabao mawili wakati Real Madrid iliposhinda mabao 2-1 dhidi ya Sporting Gijon.
Lakini kikubwa kilicholeta mjadala kwenye mchezo huo sio matokeo ya mchezo bali ni jezi walizovaa Real Madrid.
Real Madrid waliingia uwanjani na jezi ambazo zilikuwa zinaangaza, hali iliyozua mjadala mkubwa kwa wadau wa soka ulimwenguni.
Sababu kubwa ya kufikia uamuzi huo kwa mabingwa hao watetezi wa Champions League ni suala la uhifadhi wa mazingira.
Fulana za jezi hizo zimetengeneza na plastiki nyembamba iliyotokana na chupa zilizotupwa katika Bahari ya Hindi na baadaye kuyayushwa na kutengenezwa jezi na Adidas.
Kila jezi ilitengenezwa kwa kutumia chupa 28 zilizoyayushwa. Adidas wanapambana kwa kushirikiana na Parley ambao ni wanaharakati wa masuala ya bahari, ambao wana nia ya kuongeza ufahamu kwa watu kuhusu utunzaji na matumizi bora ya vyanzo vya maji ambavyo kwa sasa vinaathiriwa sana na matumizi yasiyo sahihi.
Wakati fulani Bayern Munich walitengenezewa jezi hizo lakini sehemu ya kitambaa cheusi kililetea ugumu kwa mabingwa hao watetezi wa Bundesliga, kabla ya zoezi hilo kuhamishiwa kwa Real Madrid!

Source:shaffihdauda

Jiunge na hatukwamii.blogspot.com/ sasa
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video


0 comments:

Post a Comment