Monday, November 28, 2016

RAIS DKT MAGUFULI APOKEA MARAIS WA ZAMBIA NA CHAD JIJINI DAR

Mheshimiwa Idriss Deby Itno, Rais wa Jamhuri ya Chad na Mwenyekiti wa sasa wa Umoja wa Afrika atakuwa na ziara ya kikazi nchini Tanzania tarehe 27-28 Novemba, 2016.
Mheshimiwa Rais Deby amewasili na kupokelewa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) mjini Dar es Salaam na kulakiwa na Mwenyeji wake Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muugano wa Tanzania. Aidha, Mheshimiwa Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Viongozi wengine waandamizi wa Serikali ya Tanzania walikuwepo Uwanja wa ndege katika mapokezi hayo.

c1
 Rais wa Jamhuri ya Chad Mhe Idriss Deby Itno akipokea shada ya maua  mara  baada ya kiongozi huyo kuwasili katika uwanja wa  ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam jana jioni Novemba 27, 2016
Akiwa hapa nchini, Mheshimiwa Rais Deby na Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki watakuwa na mazungumzo rasmi Ikulu, ambapo watapata fursa ya kubadilishana mawazo kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu ya Ukanda wa Afrika Mashariki na Umoja wa Afrika kwa ujumla.
Mheshimiwa Rais Idriss Deby ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika kwa Mwaka 2016-2017, kipindi ambacho Umoja huo umeendelea kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazoikabili bara letu, zikiwemo ugaidi, amani na usalama, na changamoto za maendeleo Barani Afrika.
c2
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Dkt John Pombe Magufuli amlaki  mgeni wake  Rais wa Jamhuri ya Chad Mhe Idriss Deby Itno mara  baada ya kiongozi huyo kuwasili katika uwanja wa  ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Novemba 27, 2016.
Ujumbe wa Rais huyo pia unawajumuisha Mke wa Rais Mama  Hinda Deby Itno, Mheshimiwa Moussa Faki Mahamat, Waziri wa Mambo ya Nje, Mtangamano wa Afrika, na Ushirikiano wa Kimataifa wa Chad na viongozi wengine waandamizi wa Serikali ya Chad.
c3
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Dkt John Pombe Magufuli akimtambulisha  na mgeni wake  Rais wa Jamhuri ya Chad Mhe Idriss Deby Itno kwa viongozi wa vikosi vya ulinzi na usalama mara  baada ya kiongozi huyo kuwasili katika uwanja wa  ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Novemba 27, 2016.
c4
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Dkt John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake  Rais wa Jamhuri ya Chad Mhe Idriss Deby Itno mara  baada ya kiongozi huyo kuwasili katika uwanja wa  ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Novemba 27, 2016.
c6
c7
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Dkt John Pombe Magufuli akimzwadia kinyago cha Kimakonve cha “Umoja” na picha ya kuchora ya tembo na Mlima Kilimanjaro na mgeni wake  Rais wa Jamhuri ya Chad Mhe Idriss Deby Itno mara baada ya kiongozi huyo kuwasili  kwa mazungumzo Ikulu  jijini Dar es salaam, Novemba 27, 2016
c8
z1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Dkt John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake  Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Chagwa Lungu mara  baada ya kiongozi huyo kuwasili katika uwanja wa  ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Novemba 27, 2016.
z3
z4
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Dkt John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake  Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Chagwa Lungu wakisimama kwa ajili ya nyimbo za Taifa na mizinga 11 mara  baada ya kiongozi huyo kuwasili katika uwanja wa  ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Novemba 27, 2016
z5
Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Chagwa Lungu akikagua gwaride rasmi mara tu baada ya kupokewa na mwenyeji wake Rais Dkt John Magufuli katika uwanja wa  ndege wa kimataifa wa 
Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Novemba 27, 2016.
z6
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Dkt John Pombe Magufuli akimtambulisha Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Chagwa Lungu kwa Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa baada ya kuwasili katika uwanja wa  ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Novemba 27, 2016.
z7
Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Chagwa Lungu akisalimiana na mabalozi wanaowakilisha nchi mbalimbali za Afrika nchini mara tu baada ya kupokewa na mwenyeji wake Rais Dkt John Magufuli katika uwanja wa  ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Novemba 27, 2016.(Picha zote na IKULU).



Source:dewjiblog

Jiunge na hatukwamii.blogspot.com/ sasa
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video





0 comments:

Post a Comment