Wednesday, June 7, 2017

Manchester United waiondoa Real Madrid kileleni mwa klabu tajiri duniani.

Wakati Toni Kroos anasajiliwa Real Madrid alisema klabu kubwa duniani ziko nne ambazo ni Real Madrid,Bayern Munich,Barcelona na Manchester United hiyo ikitokana na historia za klabu hizo lakini pia utajiri na mafanikio yao.

Manchester United hawakucheza Champions League msimu uliopita, na msimu huu wamemaliza nje ya nafasi nne za juu katika ligi kuu ya nchini Uingereza lakini hilo sio tatizo kwao hata kidogo katika masuala ya kifedha.
Baada ya miaka mitano kupita klabu ya Manchester United imerejea kileleni mwa klabu ambazo zinaongoza kwa thamani kubwa kifedha kutokana na utafiti uliofanywa na jarida maarufu la Forbes.
Pamoja na majanga yanayoendelea kukumba klabu hiyo ndani ya uwanja lakini thamani ya United imeongezeka kwa 11% zaidi ya mwaka jana ambapo sasa United wana thamani ya $3.69b wakiwa juu ya miamba ya nchini Hispania ya Real Madrid na Barcelona.
Thamani ya United inatokana na mauzo ya tiketi pamoja na haki za matangazo na mambo mengine ikiwemo mauzo ya jezi, chini ya Manchester United kuna klabu ya Barcelona ambayo thamani yake ni $3.64b.
Pamoja na Real Madrid kufanikiwa kutwaa ubingwa wa Champions League na La Liga lakini thamani yao kibiashara imepungua kwa 20% na katika orodha ya vilabu vyenye thamani duniani kifedha wameanguka hadi nafasi ya tatu wakiwa na thamani ya $3.58b.
Mabingwa wa nchini Ujerumani Bayern Munich nao wapo katika nafasi ya nne ambapo wana thamani ya $2.71b mbele ya matajiri wengine wa jiji la Manchester klabu ya Manchester City wenye thamni ya $2.08bilion.
Arsenal ambao wanaonekana mabahili sana katika suala zima la usajili wanashika nafasi ya tatu nchini Uingereza kwa kuwa na thamani kubwa huku wakiwa nafasi ya sita duniani wakiwa na thamani ya $1.93b mbele ya mabingwa wa nchini Uingereza Chelsea walioko nafasi ya saba na thamani ya $1.85b.
Liverpool wako katika nafasi ya nane wakiwa na thamani ya $1.49b wakifuatiwa na klabu ya Juventus ambao thamani yao ni 1.26b na Tottenham Hotspur wakimalizia nafasi ya 10 ya vilabu vyenye thamani Ulimwenguni wakiwa na thamani ya 41.06B.
source:shaffihdauda
Tuandikie Maoni Yako Hapa Chini. Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video za kufurahisha na kuvunja mbavu.

0 comments:

Post a Comment