MWILI wa Spika mstaafu wa Bunge, Samuel Sitta ambaye alifariki dunia juzi nchini Ujerumani, utawasili nchini kesho alasiri.
Mwili wa Sitta ambao utazikwa siku ya Jumamosi huko Urambo, utaagwa na wananchi wa jijini Dar es Salaam ambako alikuwa akiishi, Dodoma ambako aliishi akiwa Spika wa Bunge na mjini Urambo ambako ndiko nyumbani alikokulia na kuwa mbunge wa jimbo hilo kwa nyakati tofauti.
Aidha, imefahamika kwamba mwili wa Sitta utazikwa katika kitongoji cha Mwenge wilayani Urambo, eneo ambalo mwanasiasa huyo aliandaa kwa ajili ya ndugu kuzikwa.
Awali, kulikuwa na taarifa kwamba angezikwa eneo la Utemini la Wanyanyembe huko Itetemia katika Manispaa ya Tabora, kwa kuwa wamezikwa ndugu zake wengine na ndiko anakotokea mama yake, Hajjat Zuwena Said Fundikira wa ukoo wa Chifu Fundikira.
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na msemaji wa familia, Gerard Mongola, mwili wa Sitta utawasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere saa 8.30 mchana.
“Baada ya kuwasili, mwili utapelekwa nyumbani kwake Masaki, Dar es Salaam na utalala huko hadi kesho yake siku ya Ijumaa ambako utapelekwa katika uzikwe eneo ambalo Sitta aliandaa kwa ajili ya ndugu kuzikwa”.
Source:mtembezi
0 comments:
Post a Comment