Wednesday, October 5, 2016

WALICHOKIFANYA NAVY KENZO NA ALIKIBA..

Baada ya KAMATIA CHINI pamoja na nyimbo ya GAME kupenya katika mipaka ya Afrika mashariki na Afrika kwa ujumla kundi matata la muziki kutoka TANZANIA linaloundwa na couples wawili AIKA pamoja na producer bora wa mwaka 2015-2016 NAHREEL wameingia jikoni na kupika hits nyingine kibao ikiwemo colabo ambayo tayari imefanywa pamoja na ali kiba


Miezi kadhaa nyuma Navy kenzo walitoa mipango yao ya kufanya colabo na wasanii kutoka nje ya mipaka ya TANZANIA akiwemo PATORAKING na wengine kibao
 “Mmmh tuna nyimbo nyingi ukiacha hii na Ali kiba na tayari tuna nyimbo ambayo tumesha shoot South Africa kwa Justin compus na ipo tayari kabisa vile vile tuna colabo kibao kutoka nje ya mipaka ya TANZANIA ikiwemo NIGERIA pamoja na South Afrika hivyo nadhani ni muda wa mashabiki wetu kusubiri coz tumeandaa vitu vizuri kwa ajili ya kufunga nao mwaka.” alisema AIKA
Lakini pia Navy kenzo limekuwa kundi pekee ambalo limechaguliwa kutoka TANZANIA kupeperusha bendera  kwenye msimu mpya wa nne wa COKESTUDIO AFRIKA ambayo inafanyikia nchini kenya
 Vile vile kundi hilo limekuwa nominated katika tuzo mbili  kubwa AFRIKA MTV MAMA zitazofanyika october 22 SOUTH AFRICA ukumbi wa ticket pro Dome pamoja na wats up tv africa video music award 2016 za GHANA

0 comments:

Post a Comment