Thursday, November 10, 2016

Cristiano Ronaldo apata mkataba wa kudumu kutoka...........

Baada ya kusaini mkataba wa miaka mitano na Real Madrid, Cristiano Ronaldo ametangaza kuongeza mkataba wake na Nike. Kupitia video iliyotolewa Beaverton Oregon Marekani ambako ni makao makuu ya kampuni hiyo ya vifaa vya michezo, Ronaldo ameeleza kuwa mkataba huo ni wa maisha, huku akiisifu Nike kwa ubunifu wao.
Akiwa na furaha Ronaldo ameisifu Nike kuwa ni kampuni inayofanya mambo ambayo hakuna kampuni nyingine inafanya. Mkataba huo mnono utakuwa unamwingizia Euro 20 milioni kwa mwaka sawa na bilioni zaidi ya 60 za Tanzania.

Ronaldo sasa amefuata nyayo za nyota wa kikapu nchini Marekani LeBron James ambaye Desemba mwaka jana alisaini mkataba wa maisha na kampuni ya Nike unaomfanya kukusanya kiasi cha $500 milioni.

Mbali na mkataba na Nike Ronaldo mwenye miaka 31, hivi karibuni ameongeza mkataba wake na Real Madrid hadi 2021.




Source:mtembezi

Jiunge na hatukwamii.blogspot.com/ sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video




0 comments:

Post a Comment