Hakuna kitu ambacho mashabiki wa Diamond na Wema wanakipenda kama kuwaona wawili hao wakishirikiana bila matatizo na wenyewe wameamua kufanya kama mashabiki wao wanavyopenda.
Mbali ya siku za hivi karibuni wawili hao kuonekana wakishirikiana na kupeana support kwenye mambo mbalimbali, Diamond na Wema kwasasa ni marafiki na wanawasiliana mara kwa mara, Diamond amemwaga ubuyu.
Akizungumza kwenye kipindi cha ‘The Playlist’ Diamond amesema kuwa japo kiukweli mwanzoni walikuwa hawapatani lakini kwasasa yeye na mpenzi wake wa zamani hawana matatizo kabisa na huwa wanawasiliana na kushauriana vitu vya kimaendeleo,
“Ofcourse mimi na wema tulikuwa na tatizo, kwasababu watu mnavyokuwa kwenye mahusiano mnapoachana lazima kuna kuwa na vitatizo fulani hivi, so matatizo yanaendaga lakini baadae mnakuwa mnapevuka, so inafika time yanaisha, so imefika time yameisha tumekuwa wana hata wakati nakuja kabla sijafaika hapa, nilikuwa nazungumza nae” Diamond alifunguka.
Pia Diamond amesema mpenzi wake wa sasa, Zari hana tatizo lolote kuhusu yeye kuwa na ukaribu na mpenzi wake wa zamani.
0 comments:
Post a Comment