Waziri wa elimu,sayansi na teknolojia na mafunzo ya ufundi, Profesa Joyce Ndalichako, amesema baada ya serikali kumaliza ujenzi wa maabara sasa serikali imeanza kununua vifaa vya maabara kwa ajili ya shule za sekondari nchini.
Akizungumza na jumuiya ya shule ya sekondari ya Iyunga akiwa katika ziara yake ya siku tatu mkoani humo, Prof Ndalichako amesema kuwa vifaa hivyo vimenunuliwa kwa gharama ya shilingi bilioni 12.
“Nafurahi kwamba tumeleta fedha,kama serikali na hiyo fedha inatumika vizuri katika kufanya jambo ambalo limekusudia na nimeona nyuso za furaha kutoka kwa walimu, kutoka kwa wanafunzi kwakweli wanafurahi kuona miundo mbinu yao inafanyiwa ukarabati. alisema.
“Vifaa tulivyoagiza thamani yake ni kama bilioni 12, kwahiyo ni vifaa vingi unaweza ukaona ilikuwa ni international tender. Kama sikosei kuna vifaa vingine vitakuwa vinatoka kama Urusi vingine vinatoka Uingereza,lakini vinategemea kufika mwishoni mwa mwezi wa 11 kwasababu ya ule mchakato wa kuvisafirisha mpaka kuvileta,” alifafanua.
“Hatukupenda kumpa tenda kubwa mtu mmoja,ukiweka mayai yako kwenye kitu kimoja kikitokea kitu chochote inakuwa ni shida. Kwahiyo vimegawanywa kwa mafungu na kwa mujibu wa mkataba tunatarajia mwezi wa 11.”
BY: EMMY MWAIPOPO
Jiunge na hatukwamii.blogspot.com/ sasa
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video
0 comments:
Post a Comment