Sunday, October 16, 2016

Hapi afanya ziara Mabwepande, apiga marufuku uuzaji wa pombe mida ya kazi


Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi jana aliendelea na ziara yake katika Kata ya Mabwepande ambako alishiriki kikao cha maendeleo ya kata (WADC) na kuzungumza na wazee wa kata hiyo pamoja na kufanya mkutano wa kusikiliza kero za wananchi.
Katika ziara yake hiyo, Mkuu wa wilaya alipokea kero mbalimbali za wananchi ikiwemo uvamizi wa ardhi, changamoto za soko la Bunju, ulinzi na usalama na kero ya maji.
Akieleza dhamira yake katika hatua mbalimbali Hapi aliwaambia wananchi wa Mabwepande kuwa tayari suala la uvamizi wa ardhi limeanza kufanyiwa kazi ili kupatiwa suluhu ya kudumu.
Kuhusu baadhi ya wafanyabiashara wa soko la Bunju kupanga bidhaa zao barabarani hali inayowafanya wenzao walioko ndani ya soko kutofanya biashara, Hapi ameagiza kuwa ifikapo jumatatu ijayo wafanyabiashara wote walioko barabarani waondolewe na kwenda katika soko rasmi.
Wananchi wa Bunju walimshukuru Mkuu wa wilaya kwa kuwatembelea na kumsihi kuyafanyia kazi yote waliyomwambia.
Hapi amewasisitiza viongozi na watendaji wa kata na mitaa kufanya kazi kwa bidii na maarifa, kudhibiti uuzwaji wa Pombe saa za kazi na kuimarisha vikundi vya ulinzi shirikishi.


Jiunge na hatukwamii.blogspot.com/ sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video 




0 comments:

Post a Comment