Thursday, September 29, 2016

Rapper wa Bongo ambaye Nay wa Mitego humsikiliza zaidi

Kwa muda mrefu kumekuwepo na mjadala kwenye jumuiya ya hip hop ya Tanzania kuhusu iwapo Nay wa Mitego anafanya muziku huo ama la.

Mdahalo huo ulikuzwa zaidi miaka miwili iliyopita baada ya Nay kunyakua tuzo ya hip hop kwenye KTMA.

Hata hivyo staa huyo pamoja kufanya muziki wenye ladha tofauti wakati mwingi, anaamini kuwa hip hop ndio kitu anachokifanya. Na ile kuwepo kwenye boti moja na wajuzi wa muziki huo, hana budi kumsikiliza mjuzi zaidi wa miondoko hiyo kuwahi kutokea katika ardhi ya Mwalimu Nyerere.
Nay amedai kuwa humsikiliza zaidi Fareed Kubanda aka Fid Q. Alisema hayo kwenye kipindi cha Ngaz Kwa Ngaz alipoulizwa ni msanii gani anayemsikiliza sana.
Collabo kati yao inaweza kuwa na kishindo kikubwa.

0 comments:

Post a Comment