Thursday, September 29, 2016

DIAMOND PLATNUMZ AZUNGUMZA KUHUSU KUWASAIN BELLE 9 NA BILLNASS KATIKA LEBEL YA WCB


Baada ya kusikika kwa tetesi kwamba Belle 9 na Billnasi kwamba wamejiunga na WCB, Sasa Diamond platnumz ameamua kufunguka juu ya hilo.
List ya Wasanii walio chini ya record label ya WCB Wasafi records Baby, kuna Diamond Platnumz mwenyewe CEO, kuna Harmonize, Ray Vanny, Rich Mavoko pamoja na mtoto wa kike wa mwanamuziki Veteran wa Taarabu Khadija Kopa Omar.
Lakini hivi karibuni kuna rumors zinadai kuwa lebel hiyo yenye makao yake makuu pande za sinza imewa sign rapper Billnas pamoja na hit maker wa burger movie selfie mtu mzima Belle 9, Sasa je huu ubuyu ni wa kweli?, Mtu mzima Diamond akatusanukia ishu nzima.
Akiongea na Perfect255, Diamond Platnumz amesema kwamba bado wasanii hao hajawasign kwani anaamini kwamba kumsign mtu ni biashara, kwahiyo Diamond platnumz amefunguka kwamba labda kama itokee kwa Meneja wake wawe wamefanya hivyo, lakini yeye amesema kwamba hajawasign wasanii hao.

0 comments:

Post a Comment