Kukua kwa teknolojia ya simu za Smartphone kumekuja na changamoto kubwa kwa baadhi ya makampuni yanayotengeneza simu za mkononi. Kampuni ya Blackberry ni moja kati ya makampuni yaliyokiri kupata hasara kubwa baada ya kushindwa kwenda sawa na mahitaji ya wateja wake.
Blackberry imekiri kupoteza kiasi cha dola za Marekani milioni 372 baada ya simu yake mpya aina Q2 kutofanya vizuri baada ya kuingizwa sokoni, Hasara hiyo imepelekea kampuni ya Blackberry kutangaza kuacha kutengeneza simu za Smartphone.
Ikumbukwe kuwa BlackBerry ndio kampuni ya kwanza duniani kutengeneza simu za Smart, kutoka nchini Canada, ambao wametangaza maamuzi hayo jana September 28, 2016, na kuliacha jukumu hilo kwa kampuni rafiki ya PT Tiphone Mobile Indonesia Tbkkutoka Indonesia, ambapo wao wataendelea na kazi ya kubuni software na huduma muhimu za simu hiyo.
Pamoja na kuwa moja kati ya makampuni ya kutengeneza simu yaliyofanya vizuri miaka kadhaa iliyopita Kampuni hiyo imejikuta ikiendelea kushuka kwenye soko kwa speed ilipoamua kutumia dola milioni 372 mpaka mwezi August 31, 2016 kisha ikaingiza dola milioni 334 tu na kuachwa mbali na kamouni za Apple na Android.
0 comments:
Post a Comment