Thursday, September 29, 2016

Chris Brown amethibitisha kufanya show kwenye nchi hii Afrika Mashariki


Siku chache baada ya kuondoka star Trey Songz aliyekuja Afrika Mashariki katika nchi ya Kenya kwenye msimu wa Coke Studio Afrika unaofanyika jijini Nairobi, Hii ni good news tena kwako shabiki wa muziki wa R&B kutoka kwa star wa single ya Sexy U Back To Sleep Chris Brown amethibitisha kuwa ataingia nchini Kenya mwezi ujao.


Star huyo wa muziki wa Hip Hop na R&B atafanya show yake ya kwanza nchi Kenya katika ukumbi wa Mombasa Golf Club wiki ijayo, October 8, 2016. Tamasha hilo litawakutanisha wasanii ambao kwasasa wamekua marafiki zaidi, Wizkid kutoka Nigeria atakayepanda steji moja na Chris Breezy just imagine itakuaje mtu wangu.
Chris Brown amecomfirm kuja kwake Afrika Mashariki kupitia Video fupi iliyopostiwa kwenye mtandao wa YouTube, akiwataka Wakenya wajitokeze kwa wingi siku hiyo.
“Yoyo 001, Mombasa Kenya, can’t wait to come out there. Kenya we are turning it up. October 8th make sure you’re there, make sure you’re ready and we are gonna party, thank you,” anasikika mshindi huyo wa tuzo ya Grammy Award.
Wakenya watapata nafasi ya kumshuhidia Breezy kwenye stage kwa kiingilia cha shilingi 10,000 za Kenya kwa tiketi za kawaida huku VIP ikiwa shilingi 20,000 na VVIP itakua shilingi 50,000 za Kenya.

0 comments:

Post a Comment