Monday, May 22, 2017

Rekodi ilizoweka Real Madrid baada ya kutwaa La Liga

Mabao mawili ya Cristiano Ronaldo na Karim Benzema yaliiwezesha Real Madrid kutwaa taji la kwanza la La Liga tangu 2012 katika ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Malaga.
Cristiano Ronaldo alifunga bao la kuongoza dakika ya kwanza huku Karim Benzema akiongeza bao la pili baada ya mapumziko katika mchezo ambao Real Madrid walihitaji pointi moja tu kutwaa ubingwa.
Real Madrid ilimaliza mbio zake za bila kutwaa ubingwa (misimu minne) tangu 1994 huku pia ikiweka rekodi ya kufunga mabao kwenye kila mechi katika michezo yote ya msimu mmoja wa La Liga kwa mara ya kwanza.
Hadi inacheza mchezo wa mwisho kumaliza msimu wa La Liga Real Madrid imefunga mabao 58 ugenini ikiwa ni rekodi yao bora kwenye msimu mmoja wa La Liga huku pia ikiweka rekodi ya kufunga mabao kwenye mechi 64 za mashindano yote – rekodi bora kwao ukilinganisha na timu za Ligi kubwa tano za Ulaya.
Cristiano Ronaldo ni mfungaji bora wa muda wote kwenye Ligi kuu tano za Ulaya (369), akimzidi Jimmy Greaves (366)
Zinedine Zidane anakuwa mchezaji wa zamani wa sita wa Real Madrid kushinda La Liga akiwa meneja, baada ya Bernd Schuster, Vicente del Bosque, Jorge Valdano, Luis Molowny na Miguel Munoz.

source:millardayo
Tuandikie Maoni Yako Hapa Chini. Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video za kufurahisha na kuvunja mbavu.

0 comments:

Post a Comment