Serengeti Boys imeyaaga mashindano ya AFCON U17 huko Gabon baada ya kufungwa bao 1-0 na timu ya taifa ya vijana ya Niger kwenye mechi ya mwisho ya Kundi B.
Ilihitaji kupata sare ya aina yoyote ili kufuzu atua ya nusu fainali ya mashindano hayo ambapo ingekua imekata tiketi ya kucheza mashindano ya kombe la Dunia kwa umri huo.
Goli lililoitupa nje Serengeti Boys limefungwa dakika ya 42 kipindi cha kwanza lakini kabla ya ilionekana mpira ulitoka kabla ya Marou kuucheza kisha kumgonga beki wa Serengeti na kujaa wavuni.

Serengeti imemaliza katika nafasi ya tatu ikiwa na pointi nne nyuma ya vinara Mali yenye pointi saba huku Niger ikiwa na pointi nne sawa na Tanzania lakini Niger wanasonga mbele kwa sababu wameifunga Tanzania kwenye mechi ya wenyewe kwa wenyewe.
Angola imepoteza mechi yake ya mwisho kwa kufungwa 6-0 na Mali hivyo inaungana na Tanzania kuaga mashindano hayo na kuziacha Mali na Niger zikisonga mbele kucheza nusu fainali.
source:shaffihdauda
Tuandikie Maoni Yako Hapa Chini. Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video za kufurahisha na kuvunja mbavu.
0 comments:
Post a Comment