Thursday, June 8, 2017

Messi akiri “Ronaldo hafai”

Kwa kizazi chetu cha sasa ukimuuliza kijana yoyote ni yupi mchezaji bora wa dunia yatakuja majina mawili tu Cristiano Ronaldo na Lioneil Messi kutokana na kiwango wanachoonesha siku za karibuni, hii inatokana na tuzo binafsi pamoja na makombe ambayo wamekuwa wakibeba siku za usoni.
Lakini katika miaka hii miwili mfululizo Cristiano Ronaldo ameonekan bora zaidi ya Messi kwani ameisaidia Ureno kubeba kombe la Ulaya mwaka jana pia akasadia Real Madrid kubeba kombe la Champions League msimu uliopita na akafanikiwa kutetea kombe hilo wiki iliyopita na akiipa Madrid kombe la La Liga.
Sasa mpinzani wake wa karibu ambaye ni Lioneil Messi ameulizwa kuhusu tofauti yake na Ronaldo ambapo Messi amesema yeye na Ronaldo wako poa tu akini kila mtu anajaribu kupambana ili kuonesha alichonacho uwanjani ila nje ya uwanja hakuna tofauti kati ya nyota hao wawili.
Kuhusu uwezo wa Ronaldo uwanjani Lioneil Messi amesema Ronaldo ni “bora sana” alisema “tunajaribu kufanya kitu bora kwa ajili ya timu zetu kila mwaka lakini kuhusu nje ya uwanja sifikirii sana kama hilo ni muhimu,dunia nzima inajua kuhusu Ronaldo ni mcheza bora na ndio maana ni mmoja kati ya wachezaji bora duniani.”
Lakini pia Messi alizungumzia taarifa za kuongeza mkataba mpya ndani ya Barcelona ambao utaisha mwaka 2021 akisisitiza ya kwamba hana mpango wa kuondoka Nou Camp na anataka kumalizia maisha yake ya soka katika uwanja huo kwani hilo ndiop jambo ambalo amekuwa akiliota kila siku.

source:shaffihdauda
Tuandikie Maoni Yako Hapa Chini. Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video za kufurahisha na kuvunja mbavu.



0 comments:

Post a Comment