Monday, May 22, 2017

JPM na Museven Wasaini Mkataba wa Ujenzi wa Bomba la Mafuta.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Uganda jana wamesaini mkataba wa ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Hoima Uganda mpaka Tanga Tanzania chini ya Rais John Magufuli na Yoweri Museveni ikulu jijini Dar es salam.

Akizungumza baada ya kutia saini tamko hilo Mhe. Rais Magufuli amemshukuru Mhe. Rais Museveni kwa hatua ambayo Tanzania na Uganda zimefikia katika mradi wa bomba la mafuta la Hoima – Tanga na ameeleza kuwa mradi huo ni matokeo ya urafiki na undugu wa kihistoria uliopo kati ya nchi hizi mbili.

“Kwa hiyo mimi nakushukuru sana Mhe. Museveni na kwa niaba ya Watanzania wote tumefurahi sana, umetengeneza historia ya Tanzania na Uganda na pia umeimarisha uhusiano na ushirikiano mzuri uliopo kati ya nchi zetu, Watanzania hawatakusahau” amesema Mhe. Rais Magufuli.

Kwa upande wa Rais Museven ambaye ni mmoja wa wafuasi wa Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere aliyepigania ukombozi wa nchi mbalimbali za Afrika na aliyekuwa na ndoto ya kuiunganisha Afrika nzima zao ili kujipatia manufaa ya kiuchumi, ametoa wito kwa viongozi hasa vijana kuendeleza misingi ya umoja na ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.

"Nimefurahi sana leo, najua kuna kazi kubwa imefanyika hadi kufikia hatua hii, lakini hii pia imeonesha kuwa na sisi tunaweza” amesema Mhe. Museveni.

Tanzania na Uganda (Inter-Governmental Agreement–IGA) ambao umepangwa kukamilika katika kipindi cha wiki moja, na baada ya hapo taratibu za kuweka jiwe la msingi la kuanza kwa ujenzi wa mradi huo zitafanyika.

Ujenzi wa mradi wa bomba la mafuta ghafi la Hoima – Tanga wenye urefu wa jumla ya Kilometa 1,443 zikiwemo 1,115 zitakazojengwa ndani ya ardhi ya Tanzania utagharimu Dola za Marekani Bilioni 3.55, unatarajiwa kusafirisha mapipa laki 2 ya mafuta kwa siku na wakati wa ujenzi unatarajiwa kuzalisha ajira kati ya 6,000 na 10,000.


Tuandikie Maoni Yako Hapa Chini. Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video za kufurahisha na kuvunja mbavu.

0 comments:

Post a Comment