Monday, May 22, 2017

Mashabiki wa Barcelona wasema marefa wameshinda ubingwa wa La Liga.

Baada ya Real Madrid kushinda ubingwa kwa msimu unaoisha, mahasimu wao hawana furaha kabisa kama ilivyotegemewa na kila mtu. Ubingwa wa Real Madrid umeamuliwa kwa mechi moja ambapo wameshinda magoli 2-0 dhidi ya Malaga.

Kwa upande wa Barcelona mashabiki wameanza kutoa lawama kwa marefa kwa kusema wamewabeba sana Real Madrid kiasi cha kusema kwamba wao ndio wameshinda ligi na sio kikosi cha Blancons.
Mashabiki hao walizidisha kusema kwamba Ronaldo na Messi hawawezi kufananishwa kwasababu Messi ameonyesha uwezo ambao ni ngumu kabisa kufananisha na kiwango cha Ronaldo.
Kwenye mechi ya mwisho Barcelona walipata penati mbili kutoka kwa refa wao ambapo moja alikosa mchezaji wao nyota Messi.
Zinedine Zidane amekua mchezaji wa 6 kati ya wachezaji wa zamani wa Real Madrid kuiongoza Real kushindi ubingwa wa ligi, yeye pia alishinda ubingwa huu kwama 2002-03.
Hadi sasa Zidane ameshinfa makombe 4 akiwa na Real Madrid ambayo ni La Liga, Super Cup, Club World Cup na Champions League. Pia hili kombe limekua la 33 kwenye historia ya club ya Real Madrid.

source:shaffihdauda
Tuandikie Maoni Yako Hapa Chini. Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video za kufurahisha na kuvunja mbavu.

0 comments:

Post a Comment