Wasanii wa muziki waliowahi kufanya vizuri na wimbo ‘Nikupe Nini’, Mandojo na Domokaya wamemtaja AliKiba na Diamond kuwa ni miongoni mwa wasanii ambao wanatamani kufanya nao kazi.
Wakizungumza na On Point ya Clouds FM Jumapili hii, wakali hao wa zamani wamesema kuna wasanii wengi ambao wanatamani kufanya nao kazi.
“Kwanza kabisa sisi kama Mandojo na Domokaya kuna wasanii wengi tunatamani kufanya nao kazi, kama hawa wadogo zetu akina, AliKiba na Diamond. Hawa ni wadogo zetu na wao wanatukubali sana kwa sababu sisi tuliwaanzishia njia kwa hiyo hata sisi tunahitaji kufanya nao kazi ili kuchanganya ladha. Kwa hiyo kuna wasanii wengi ambao tunaweza kufanya nao kazi, Diamond, AliKiba pamoja na wengine,” alisema Mandojo.
Wawili hao ambao wanajipanga kurudi rasmi kweye game,wanafanya bishara ya viatu katika soko la Kariakoo jijini Dar es salaam.
0 comments:
Post a Comment